Mabingwa wa tetezi wa kombe la
shirikisho (FA) Yanga, wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons.
Mchezo huo wa robo fainali
umefanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo yanga
sasa inaungana na mahasimu wao Simba, Azam na Mbao FC katika hatua
inayofuata ambayo ni nusu fainali.
Yanga ilipata magoli yake kupitia
kwa Amissi Tambwe aliyefunga dakika ya 16 ya mchezo, Obrey Chirwa
akafunga bao la pili dakika ya 41 na kuifanya Yanga kwenda mapumziko
ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
Simon Msuva aliifungia Yanga bao
la tatu dakika ya 46 ya mchezo huo uliokuwa mkali kwa pande zote licha
ya kuharibiwa na hali ya uwanja kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha.
Prisons nusura wapate bao la
kufutia machozi baada ya kupata penalti dakika ya 54 lakini mpigaji
Victor Hangaya aligongesha mwamba.
Baada ya ushindi huo, Yanga
inakamilisha timu nne za nusu fainali, droo ya hatua hiyo itafanyika
kesho ilikujua timu gani zitakutana kwenye michezo ya nusu fainali.

0 Comments