Baadhi ya wananchi Kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kutembelea ujenzi wa madarasa sita ,shule ya msingi Kimele
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo wa kushoto akizungumza jambo diwani wa Kata ya Mapinga ,Ibrahim Mbonde wa katikati aliyevaa kibagharashia ,wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alhaj Majid Mwanga.
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
HALMASHAURI ya
wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,inaendelea na harakati za kukabiliana na tatizo
la upungufu wa madarasa ambapo kwasasa inajenga vyumba 60 vitakavyogharimu
sh.mil.840.
Kufuatia hatua
hiyo mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,alhaj Majid Mwanga,amechangia mabati 2,000 na
mifuko ya saruji 1,000 ili kusaidia tatizo hilo.
Hayo yalisemwa
na mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo,Ally Ally Issa,wakati mkuu wa mkoa wa
Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ,alipotembelea shule ya msingi Kimele,kata ya
Mapinga kujionea hali ya ujenzi inavyoendelea.
Ally Issa
alifafanua wamejipanga kuondoa uhaba wa madarasa ambao bado upo katika shule za
msingi na sekondari.
Alieleza kuwa vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika maeneo mbalimbali ya kata zilizopo kwenye halmashauri hiyo ,vipo hatua mbalimbali ya ujenzi.
Nae diwani wa
kata ya Mapinga,Ibrahim Mbonde,alisema kata hiyo inatekeleza miradi mitatu ya
maendeleo.
Alieleza,miradi
hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule ya msingi Udindivu, vyumba vinne vya madarasa
S/M msingi Kimele na zahanati ya Tungutungu.
Mbonde
alisema,wananchi tayari wamechangia asilimia 50 kwa kujitolea fedha na nguvu
ambapo kampuni ya Simba Motors imetoa eneo la heka 20 kati ya hizo heka tano
zinatumika kwa ujenzi wa shule na heka 15 huduma nyingine za jamii.
“Tumekubaliana
kila kaya kuchangia sh.20,000 na hadi sasa tumeshapata zaidi ya sh.mil 46
na bado tunaendelea kuchangishana ili kufikia malengo”alisema Mbonde.
Mbonde
alielezea kwamba,katika ujenzi wa S/M Kimele bado zinahitajika sh.mil 10.6
ili waezeke,S/M Udindivu mil.10.22,zahanati ya Tungutungu inahitajika mil.9.12.
Diwani huyo wa
Mapinga,alisema,kata ya Mapinga itakuwa na jumla ya shule nne za msingi mara
baada ujenzi wa hizo mbili kukamilika.
Aliwashukuru
wadau wa maendeleo katika kata hiyo akiwemo mzee Hamoud Jumaa kwa kutoa hekari
tano na kiwanda cha kusindika matunda cha Elven Agri co.ltd kinachowajengea
madarasa mawili katika shule ya msingi Kimele.
Kwa upande
wake ,mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Ndikilo,alichangia sh.mil. moja ili kuunga mkono juhudi za
wananchi.
Alibainisha
kuwa,shule hiyo inatarajia kusajiliwa mapema baada ya ujenzi kukamilika hivyo
itawapunguzia kero ya mlundikano madarasani wanafunzi wa shule ya msingi
Mtambani.
Mhandisi
Ndikilo alielezea,shule hiyo kwasasa inahemewa na wanafunzi 2,400 hivyo endapo
shule ya msingi Kimele ikianza baadhi ya wanafunzi wa Mtambani watahamia
shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya
ya Bagamoyo,alhaj Mwanga ,alichangia mifuko ya saruji 125 na mabati 60 katika
shule ya msingi Kimele ili kuongeza nguvu.



0 Comments