Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi; Prof. John Lupala akitoa ufafanuzi wa Sheria ya Mipango
Miji, Na. 8 ya Mwaka 2017.
Prof. John Lupala,
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi amewataka wanachi kuzingatia Sheria Na. 8 ya mwaka 2007 kuepuka adha
zinazotokana na kutozingatia sheria hiyo.
Akitoa ufafanuzi wa Sheria
ya Mipango Miji, namba 8 ya mwaka 2007; Prof. Lupala alisema; Sheria imetungwa
ili kutoa muongozo namna ya kupanga miji nchini. Prof. Lupala amefafanua maeneo
matatu ya Mipango katika sheria hiyo.
Mipango Kabambe/ General Planning; Mipango ambayo
huandaliwa kuongoza ukuaji wa miji kwa muda wa miaka 20. Ambapo sheria
inasisitiza ushiriki wa maoni ya Wananchi.
Mipango Kina; Mgawanyo wa
viwanja au shamba unaofanywa katika eneo fulani, hutakiwa kuandaliwa kulingana
na taratibu za viwango vya upangaji ndani ya miji, alieleza hata kama mpangaji
binafsi anatumika ni lazima viwango vya kisheria vizingatiwe.
Urasimishaji; Unalenga kutambua
miliki za watu, kutengeneza viwanja vya milki za maeneo yao na kupangilia miji kwa
kuweka huduma za msingi au miundombinu ya msingi kama; maji, barabara n.k.
Pro.Lupala alisema iwapo mwananchi
hatazingatia taratibu za uendelezaji Miji bila kupata kibali cha ujenzi, Mamlaka
za Miji huchukua hatua kwa Kusimamisha ujenzi au kubomoa.
Wananchi hawana budi
kushiriki katika maoni wakati wa upangaji miji na kutojenga katika maeneo
hatarishi, ya hifadhi au oevu.
Na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi

0 Comments