Rais
Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mdahalo wakati wa
Mkutano wa World Economic Forum for Africa unaofanyika Durban, Afrika
Kusini.
| Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini pembezoni mwa mkutano huo mjini Durban |
Mkutano
wa kiuchumi Duniani -World Economic Forum kwa Afrika umeingia siku yake
ya pili hii leo mjini Durban Afrika Kusini, lengo hasa likiwa kutafuta
namna za kukuza uchumi wa Afrika.
Mkutano
huo unaokamilika kesho unahudhuriwa na maafisa wakuu watendaji wa
mashirika mbalimbali Afrika, viongozi wa kibiashara, na pia marais wa
zamani na wa sasa barani Afrika.
Mkutano
huu wa kiuchumi unafanyika wakati ambapo bara la Afrika linakabiliwa
na kiwango cha juu cha umaskini kuliko ilivyodhaniwa hapo awali,
kutokana na miongo kadhaa ya kufaidi kiuchumi idadi chache ya watu huku
mamilioni ya wengine wakisalia fukara.
Kwa
mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la uingereza linalotoa misaada
Oxfam upo uwekekano mkubwa katika kipindi cha miaka mingine 15 ijayo
waafrika millioni 250 hadi 350 wakajipata katika hali mbaya ya kiuchumi
kutona na kuendelea kutokuwepo usawa miongoni mwao.
Hata
hivyo baadhi wanahisi hali hii imetokana na usimamizi mbaya wa
raslimali za umma na pia kuwepo viongozi wasiowajika swala analokanusha
vikali aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae ni mmoja wa
wanaohudhuria mkutano huo wa Durban.
Kikwete
anasema koloni za mataifa ya Afrika pia kwa kiasi fulani yamechangia
kujikokota maendeleo Afrika kwasababu ya kutotoa usadizi wa aiana yeyote
.
"Ni
kweli wakati mwingine kuna matatizo katika utawala lakini tusichukulie
kwamba kila kitu ni kutokana na matatizo yalipo kwenye utawala tunapswa
kutafakari ukumbwa wa changamoto zilizopo mengi yamekwisha fanywa na
mengi yanahitaji kufanywa.Kwa hivyo hizi ni nchi ambazo zinahitaji
kusaidiwa."
Rais
huyo wa zamani amesema tayari serikali za mataifa mbalimbali Afrika
zimechukua hatua katika kuboresha elimu katika mataifa yao. Mikakati
hiyo ni pamoja na kuboreshwa elimu kuanzia shule za chekechea,msingi
na hata vyuo vikuu ili kupunguza idadi ya watu wasio na uwezo wa kusoma
na kuandika.
"Tanzania
ilikuwa koloni la ujerumani na vilevile la Uingereza na mpaka
tulipopata uhuru wetu walikuwepo mainjinia wawili tu.Kwa hivyo
tunapokabiliwa na mahitaji makubwa elimu ikiwa miongoni mwao, utaona
matatizo yanajitokeza na hiyo ni kwasababu tulianzia chini sana na
uwekezaji wote huu unaouona katika bara la Afrika umefanyika baada ya
nchi hizi kupata uhuru."
Msichana mdogo akitafuta mabaki ya chakula katika jaa la taka.
Afrika
na ulimwengu kwa jumla Swaziland ndio nchi inayoongoza katika ukosefu
wa usawa baina ya maskini na matajiri,na kufwatwatiwa kwa karibu na
Nigheria na kisha Afrika kusini, huku mabillionea watatu wanamiliki
utajiri wa nusu ya idadi ya watu maskini ambayo ni karibu millioni 28.
Mrais
wanaohudhuria mkutano huo wa kiuchum mjini Durban ni pamoja na mwenyeji
Jacob Zuma ,Robert Mugabe wa Zimbabwe,Yoweri Museveni wa Uganda
miongoni mwa wengine.Waziri wa fedha hapa ujerumani Wolfgang Schauble
pia anahudhuria mkutano huo.




0 Comments