Wachezaji wavulana wakishindana katika mpira wa miguu.
Wachezaji wasichana wakionesha vipaji vyao katika
kusakata soka (mchezo wa mpira wa miguu) kupata timu itakayowakilisha wilaya
katika mashindano hayo.
Timu
za netiboli kutoka shule mbalimbali zikitoana jasho kupata washindi kwa ajili
ya kushindana ngazi ya mkoa.
Wavulana wakitoana jasho katika mchezo wa mpira wa
wavu.
Riadha nayo haikuwa nyuma ambapo washiriki hawa
wavulana wakishindana katika mbio ndefu na fupi zikihusisha umbali tofauti
tofauti kuanzia mita 100 hadi mita 3000.
Mchezaji wa riadha akiruka wakati wa mashindano ya
miruko ya chini ‘low jump’ wakati wa michuano hiyo.
Washiriki wasichana wakishindana katika mbio ndefu na
fupi zikihusisha umbali tofauti tofauti kuanzia mita 100 hadi mita 3000.
Wachezaji wasichana wakisakata kabumbu kupata timu
itakayowakilisha wilaya katika mashindano hayo.
Ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu,
Paul Kasanda akizungumza na wachezaji wanafunzi kutoka shule mbalimbali
washiriki wa mashindano ya UMISETA ngazi ya wilaya katika viwanja vya Shinyanga
Sekondari.
Mwalimu Nassoro Said kutoka Shule ya Sekondari Igaga
akitoa maelezo kwa timu ya riadha yam bio fupi maarufu kama wakimbiza upepo kabla
ya kuanza kushindana kukimbia.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
imezindua mashindano ya Michezo ya Sekondari Tanzania (UMISETA) kwa mwaka 2017
kitarafa katika viwanja vya shule ya sekondari Shinyanga.
Mashindano hayo yamehusisha mpira wa miguu, netiboli,
kikapu, wavu na riadha ambapo yatashirikisha shule za tarafa mbalimbali wilayani
humo ambapo washindi watashindanishwa kupata timu za wilaya.
Akizungumza na wachezaji kutoka shule za Shinyanga
sekondari, Maganzo Songwa, Mwadui ufundi, Idukilo na Mwadui Lutheran kwa niaba
ya mkurugenzi mtendaji, Ofisa elimu sekondari, Paul Kasanda aliwataka kuwa
wamoja.
Alisema pamoja na kuwa wachezaji hao wanatoka shule
mbalimbali wilayani humo wanapaswa kushirikiana na kupata ushindi pindi watakapocheza
na wilaya zingine kutafuta wawakilishi ngazi ya taifa.
Kasanda aliongeza kwa kusema kuwa michezo ni upendo, furaha,
huleta furaha na pia huweza hata kutoa ajira kama zingine endapo wachezaji
watajituma vizuri wataweza kufika mbali.
“Pamoja na kuwa ninyi ni wamoja mnatoka wilaya moja
lakini tunataka mtuoneshe ufundi wenu, vipaji na ushindani ili tupate timu bora
zitakazoshindana na wilaya zingine,” alisema Kasanda.
Mashindano ya UMISETA kiwilaya yanatarajiwa kuanza
kutimua vumbi Mei 21 ambapo kimkoa ni Mei 22 hadi Juni 5 wakati kitaifa ni Juni
6 hadi 15 mwaka huu.










0 Comments