Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya
Kinondoni, ACP Theopista Mallya akiwaonyesha wafanyakazi wa Kampuni ya
Mawasiliano ya Zantel picha iliyotumwa na wadau wa usalama barabarani
inayoonyesha matumizi mabaya ya barabara yanayofanywa na madereva wazembe. Wafanyakazi
hao walifanya ziara katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam
mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha
siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni Mkuu wa Sheria na
Manunuzi Zantel, Rehema Khalid.
Meneja wa Afya, Ulinzi na Usalama wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel,
Nashon Mudala (aliyesimama kulia) akifafanua kuhusu alama muhimu za usalama kwa
wafanyakazi wa Zantel ambazo wanatakiwa kuzizingatia pindi wanapokuwa kazini
wakati wa ziara fupi katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam
mwishoni mwa juma. Ziara hiyo ilifanywa na wafanyakazi hao mara baada ya
kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa
kazi duniani. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa
Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya, Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel,
Rehema Khalid (Kushoto) na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry
Arthur.
Askari wa Usalama barabarani, Wilaya ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia)
akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wafanyakazi wa Zantel katika
kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara
baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya
Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa kikosi
cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni ACP Theopista Mallya na Afisa
Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha
Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya (wa pili
kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Intaneti na Simu wa Kampuni ya
Mawasiliano Zantel, Hamza Zuheri alipotembelewa na wafanyakazi wa Kampuni
hiyo katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa
wiki. Wafanyakazi hao walifanya ziara hiyo mara baada ya kuhitimisha matembezi
mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin
akizungumza na wafanyakazi wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao kuhitimisha
matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.
Hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Msasani jijini Dar
es salaam mwishoni mwa juma.





0 Comments