Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza Makundi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL).
Kadhalika TFF, limetangaza timu
saba kwa kila kundi katika michuano hiyo itakayoanza Mei 28, mwaka huu
katika vituo vya Lindi, S ongwe, Tabora na Kahama mkoani Shinyanga.
Ratiba mechi za kila kituo itatolewa Mei 22, mwaka huu.
Hata hivyo, michuano ya RCL
imechelewa kuanza baada ya baadhi ya timu kushindwa kukamilisha vigezo
vya ushiriki ikiwa ni pamoja na kulipia ada ya ushiriki kwa wakati,
leseni za wachezaji kwa wakati pamoja na kuwasilisha usajili kwa wakati.
Mwisho wa kutimiza vigezo tajwa
hapo juu ilikuwa Mei 15, 2017 lakini sasa TFF imesogeza mbele hadi Mei
18, mwaka huu ili timu ziweze kukamilisha taratibu za kulipa ada ya
ushiriki na leseni za wachezaji.
Mwisho ilikuwa iwe Mei 15, 2017
lakini TFF kiungwana tu, imetoa tena siku tatu na hivyo mwisho za
kukamilisha taratibu hizo itakuwa Mei 18, mwaka huu.
Tayari Makatibu wa Mikoa
wamejulishwa hilo tangu Mei 5, mwaka huu, lakini sasa kwa timu ambazo
hazitakamilisha taratibu za kulipia ada au leseni za wachezaji
itaondolewa kwenye mashindano.
Kundi A litakuwa Mkoa wa Lindi
ambako kutakuwa na timu za Shupavu FC ya Morogoro, Silabu FC ya Mtwara,
Mbinga FC ya Ruvuma, Politan ya Dar es Salaam, Makambako Heroes ya
Njombe, Ambassador ya Shinyanga na New Generation ya Mtwara.
Kundi B litakuwa Mkoa wa Songwe
ambako timu za kituo hicho ni Kisarawe United ya Pwani, Moto Chini FC ya
Mtwara, Makanyagio FC ya Katavi, Makumba ya Dar, Boma FC ya Mbeya, Real
Mojamoja ya Iringa na Sahare All Stars ya Tanga.
Kundi C litakuwa Kituo cha Mkoa
wa Tabora ambako kutakuwa na timu za Nyanza FC ya Manyara, Nyundo FC ya
Kigoma, Eleven Stars ya Kagera, Bodaboda FC ya Arusha, Stand Misuna ya
Singida, Majimaji Rangers ya Lindi na Area C United ya Dodoma.
Kwa upande wa Kundi D ambalo
kituo chake ni Kahama mkoani Shinyanga, kutakuwa na timu za Dar City ya
Dar, Buseresere ya Geita, Ndovu Sports ya Mwanza, Usamala FC ya Simiyu,
Baruti FC ya Mara, Green FC ya Songwe na Msange FC ya Tabora.

0 Comments