Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Tao Zhang amewasili nchini kwa
ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (Mb), pamoja na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali. katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akiwa nchini, Tao Zhang, atafanya mazungumzo na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Jijini Dar Es Salaam
Aidha, Zhang atawasilisha mtazamo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)kwa
wadau hapa nchini kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo endelevu,
kuimarisha uchumi mkubwa (Macroeconomy) na kuwa na uchumi shirikishi.
Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Tao Zhang (kushoto) waklipeana mkono
walipofika katika moja ya Hoteli jijini Dar es salaam.
(Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-WFM)
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kulia) akiongozana na mweneji
wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell
Mkwezalamba (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga, muda mfupi kabla ya kuwasili
kwa Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang, katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katikati ni Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakirisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell
Mkwezalamba (kulia) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang.
Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kulia) wakifurahia jambo baada
ya kusoma habari kuhusu ujio wa Zhang hapa nchini ambapo alikiri kutoa taarifa
na kusudi la ujio wake zilizoandikwa na Gazeti la Daily News. Ni muda mfupi
baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Amina Khamis Shaabani (kushoto) wakijadili jambo kabla ya kuwasili
kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.






0 Comments