Na Daudi
Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia
Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015,450,230
kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa kwa mtambo wa
kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani wakati
akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Mhe.Dkt Faustine Engelbert leo Bungeni.
“Mtambo huu umesaidia
Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuongeza ufanisi katika kusimamia Sekta ya Mawasiliano
pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya
Mawasiliano Duniani kote”,Aliongeza Mhe.Ngonyani
Aidha kati ya pesa
izo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi bilioni
6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa ajili
ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya
hapo kahukuwa na mapato hayo.
Amesema mtambo huu
umeiwezesha TCRA kuwa na uwezo wa kusimamia mawasiliano ya simu za Kimataifa na
zile za mwingiliano,pia mtambo huo umesaidia kudhibiti mawasiliano ya Simu za
ulaghai za kimataifa na kusimamia ubora wa mitandao katika kutoa huduma bora
kwa wananchi,kudhibiti namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano nchini pamoja
na usimamiaji wa miamala ya fedha
inayopita katika mitandao ya simu hapa nchini.
“Aidha pamoja na
mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini na
kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea”Aliongeza
Mhe.Ngonyani.
Aidha Serikali
itaendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa TCRA ili waweze kuendana na kasi ya
ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hususani katika eneo hili la
kuchakata taarifa mbalimbali za huduma za mawasiliano zinazopatikana kutoka kwa
watoa huduma ili kuweza na kujiridhisha juu ya mapato yote.

0 Comments