Na
Jonas Kamaleki- MAELEZO
Viongozi
wa Dini hapa nchini wamempongeza Kamanda Saimon Sirro kwa kuteuliwa kuwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP).
Pongezi
hizo zimetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na
Haki za Binadamu kwa jamii ya dini zote, Askofu William Mwamalanga kwa niaba ya
viongozi wa dini.
Katika
mahojiano maalum, Kiongozi huyo wa dini amemuelezea IGP Sirro kuwa ni
mchapakazi na mtu makini katika utendaji wake wa kazi.
“IGP
Sirro ni mtulivu wa na ni mtu anayetafakari maamuzi yake kwa kutafakari bila
kujali presha au maagizo ya kisiasa,” Askofu Mwamalanga alisema.
Alimuelezea
IGP Sirro kuwa ni kiongozi ambaye anawashirikisha wafanyakazi wenzake na
wananchi kwa ujumla ili kuleta amani kazi ambayo huifanya kwa weledi.
Ameongeza
kuwa kiongozi huyo wa juu katika Jeshi la Polisi ni mtu mwenye kuthubutu hasa
katika vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya na ujambazi.
“Nakumbuka
Kamanda Sirro ni polisi wa kwanza kupata tuzo katika kufanikiwa kudhibiti
majambazi,”alisema Askofu Mwamalanga.
Kiongozi
huyo wa dini ametoa ushauri kwa IGP Mpya kushughulika maslahi ya askari,
vitenda kazi katika jeshi la polisi na kurudisha uhusiano mwema kati ya Jeshi
la Polisi na raia wema ambao amesema wanafikia takribani asilimia 99.
Aidha,
Askofu Mwamalanga ameshauri kuwa IGP aelekeze zaidi nguvu katika mikoa ya
Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Kagera.
Ameitaja mikoa
mingine kuwa ni Mwanza, Arusha, Kigoma, Dodoma, Pemba na Mara, mikoa ambayo
ameitaja kuwa iko kwenye hatari ya vitendo vya uhalifu.
Kamanda
Sirro ameapishwa Siku ya Jumatatu Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Baada ya kuapishwa, IGP Saimon
Sirro alikula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma.
Kabla
ya Uteuzi huo, Kamanda Sirro ambaye sasa in IGP akichukuwa nafasi aliyokuwa
nayo Kamanda Ernest Mangu, alikuwa Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es
Salaam.


0 Comments