Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga
akiongea na wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita
katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama
ambapo aliwataka wazazi kuwalinda watoto na ndoa za utotoni pamoja na
kuwasisitiza kuendeleza vipaji vyao.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya
Maendeleo ya Jamii) Bi.Deodatha Makani akiongea jambo na Mkurugenzi wa Ubora na
Maendeleo wa Taasisi isiyo ya kiserikali
ya Save the Children Amy Schmiot mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule
ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama
Bw.Timothy Ndaya akiongea na wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya 5 ya
kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya
Mji wa Kahama ambapo alieleza dhamira ya ofisi yake kuendelea kusimamia ubora
wa shule hiyo pamoja na kushughulikia changamoto zake.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya
Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia
mahafali.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga
akikata utepe kuashiria kuanza kwa mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika
shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga
akitoa vyeti pamoja na zawadi kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwendakulima
iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha
sita ya shule hiyo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya
Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni alipohudhuria
mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo
Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga
akivishwa skafu na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo
Halmashauri ya Mji wa Kahama alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita
katika shule hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga
akioneshwa baadhi ya jumbe zilizopo katika mabango zilizoandaliwa na Taasisi isiyo
ya kiserikali ya Save the Children, alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha
sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa
Kahama.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga
akiongozwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Bi.Neema Daniel iliyopo
Halmashauri ya Mji wa Kahama kupanda mti wa kumbukumbu, alipohudhuria mahafali
ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo
Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga
akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya
Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama pamoja na walimu
wao.
Na
Hassan Silayo-MAELEZO
Wazazi
nchini wametakiwa kutekeleza wajibu wao kwa watoto kwa kuhakikisha
wanawaendeleza na kuwawezesha wafanikishe ndoto zao kwa kuwaepusha na ndoa
pamoja na mimba za utotoni.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga katika Mahafali ya 5
ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya
Mji wa Kahama.
Bi.Sihaba
amesema kuwa wazazi wanajukumu la kuhakikisha wanawalea na kuwalinda kwani
wazazi wanahaki ya kisheria ya kuwalinda watoto dhidi ya viashiria vyote
vinavyoweza kuwaweka katika mazingira hatarishi.
Bi.Sihaba
aliongeza kuwa wazazi na walezi wana haja ya kushirkiana na serikali katika
kuwalinda watoto wakike kwani watoto wa kike ni nyenzo muhimu hasa kwenye
mpango wa serikali katika kuelekea uchumi wa kati kupitia viwanda.
Aidha,Bi.Sihaba
kuwa Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Elimu sura namba 33 inayotoa
katazo kumpa ujauzito motto wa shule chini ya miaka 18 hivyo wazazi wahakikishe
wanalisimamia kwa pamoja ili kuweza kufanikisha sheria.
Naye
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bw.Timothy Ndaya alieleza dhamira
ya ofisi yake kuendelea kusimamia ubora wa shule hiyo pamoja na kushughulikia
changamoto zake ili kuendana na mipango ya serikali ya awamu ya tano katika
kuipa kipaumbele sekta ya elimu.
Mkurugenzi
wa Ubora na Maendeleo wa Taasisi isiyo
ya kiserikali ya Save the Children Amy Schmiot amesema kuwa mahafali hayo ni
ishara ya ushirikiano mzuri wa wazazi,walezi pamoja na uongozi wa shule
utakaowezesha watoto hao kuvuna kile walichokipanda kwenye miaka 6 ya masomo
yao.
Mkuu
wa shule hiyo Bi.Neema Daniel alimuahidi Bi.Sihaba kuendelea kufanya vizuri
katika mitihani ya kitaifa pamoja na kuiomba serikali kuwashika mkono hasa
katika kurekebisha miundombinu ya shule hiyo ikiwamo mabweni na uzio wa shule.
Naye
Mhitimu katika mahafali hayo Rose Bryton amewataka wazazi na walezi kutekeleza
maagizo ya serikali ya kuwalinda watoto ili kuwawezesha kutimiza ndoto na
matarajio yao kielimu.
Akitoa
ushauri kwa wazazi wenzake Bi Rebecca Peter amewataka wazazi kuachana na mila
zilizopitwa na wakati za kuwaozesha watoto wa kike katika umri usiotakiwa
kisheria bali kuwaendeleza kufikia ndoto zao.
Jumla
ya wanafunzi 143 wamehitimu masomo ya kidato cha sita katika shule ya sekondari
Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama













0 Comments