Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi
Mkazi wa Kampuni ya Cheil Engineering ambayo inajenga barabara ya
Sakina-Tengeru, Bw. Shin Pil Soo (wa pili kushoto). Kulia ni Mbunge wa
Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari na wa pili kulia ni Kaimu Meneja
wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa maelekezo Kaimu Meneja wa
TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga juu ya upandaji nyasi kwenye
eneo la katikati ya barabara wakati akikagua ujenzi wa barabara ya
Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa tahadhari juu ya gema
lililopo kwenye daraja la mto Ndoruma mara baada ya kukagua ujenzi wa
daraja hilo katika barabra ya kutoka sakina hadi Tengeru jijini Arusha,
Mei 4, 2017. Kushoto kwake ni Meya wa Arusha, Bw. Calist Lazaro.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru
Mashariki, Bw. Joshua Nassari wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa
barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, bw. Mrisho Gambo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




0 Comments