Watumishi
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kanda ya Kaskazini
wakionyesha kwa Wananchi ujumbe wa bango lao katika maadhimisho ya sherehe za
Meimosi – Kilimanjaro.
Watumishi
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Dar es Salaam
wakionyesha kwa Wananchi ujumbe wa bango lao katika maadhimisho ya sherehe za
Meimosi – viwanja vya uhuru – Dar es Salaam.
Watumishi
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Dar es Salaam wakijipanga
kuanza maandamano rasmi katika maadhimisho ya sherehe za Meimosi – viwanja vya uhuru – Dar es Salaam.
Watumishi
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Dar es Salaam (Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya
Ardhi) wakionyesha kwa Wananchi ujumbe wa bango lao katika maadhimisho ya
sherehe za Meimosi – viwanja vya uhuru – Dar es Salaam.
Watumishi
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Dar es Salaam wakifurahi
wakati wa maadhimisho ya sherehe za Meimosi yakiendelea – viwanja vya uhuru –
Dar es Salaam
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imeendelea kutahadharisha umma kuhusu umuhimu wa ulipaji wa
Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati, katika maadhimisho ya sherehe za Meimosi mkoani
Moshi, ambapo sherehe hizo zimeazimishwa rasmi kitaifa. Na Dar es Salaam katika viwanja vya Uhuru.
Kutokana na Wizara kuendelea
kuwahimiza Wamiliki wa Ardhi kulipa kodi ya pango la Ardhi, Watumishi hao
wameona ni wakati muafaka kuendelea kutangaza ujumbe huo kwa mabango katika
kuadhimisha sherehe za Meimosi.
Aidha, Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Mhe. William Lukuvi amesema; ambaye hajalipa Kodi ya Pango la Ardhi, alipe kabla ya
mwisho wa mwezi wa sita (6), kwakuwa ifikapo tarehe 30/06 hatua zifuatazo
zitachukuliwa dhidi yao;
Watashitakiwa Mahakamani, Mali zao zitakamatwa na
majengo yatapigwa mnada kupitia madalali na Miliki zao zitafutwa kwa mujibu wa
Sheria.
Na
kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi






0 Comments