Droo ya mwisho ya promosheni ya ‘Hamasika na
Masika”iliyokuwa inaendeshwa na kampuni ya kijerumani ya kuunganisha na kuuza vifaa vya nishati
inayotokana na nishati ya jua ya Mobisol yenye makao yake nchini mjini Arusha
imefanyika jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki ambapo,Bw.Baraka Mbale kutoka mkoani Mbeya amejishindia zawadi kubwa ya promosheni ya Pikipiki mpya ya Boxer.
Promosheni hiyo ya “Hamasika na Masika’ ilianza mwezi
Aprili na kumalizika leo tarehe moja Juni ambapo ililenga kuwapa nafasi za kushinda zawadi mbalimbali
wateja wapya wa Mobisol pamoja na wateja wa zamani ambao wamewashawishi wateja
kununua mitambo bora ya Mobisol. Katika
droo zilizofanyika awali jumla ya washindi sita waliweza kupatikana
katika droo mbili za mwanzo, ambapo walijishindia zawadi mbalimbali kama Redio
ya Sola, Mashine za kunyolea nywele, pamoja na pesa taslimu.
Kampeni hii imekuwa na hamasa kubwa kwa wananchi
ambapo taarifa za droo za mwanzoni zilizofanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya
Taifa ya Michezo ya Kubahatisha zinaonyesha kuwa zaidi ya wateja 3000
wameshiriki.
Bw.Baraka Mbale akiongea kwa furaha baada ya kupigiwa
simu kuwa amejishindia pikipiki mpya alisema“Kwa kweli siamini macho yangu kama
nimeshinda zawadi kubwa hivyo, maana ni sawa na nimepewa mtambo wa Mobisol bure
kabisa. Ninayo furaha sana leo, na naamini hii itakuwa chachu hata majirani
zangu kununua mtambo wa Mobisol”
Mwakilishi wa Mobisol
mkoani wa Dar e salaam,ndugu
Allan Rwechungura amesema kuwa ushiriki
huo wa wananchi wengi unadhihirisha
ni kwa jinsi wanaiamini kampuni ya Mobisol ambayo imejikita katika
utoaji wa mitambo ya sola kwa malipo ya pesa taslimu, ama kwa mkopo hadi wa
miaka mitatu.
“Nawashukuru sana wateja wote wa Mobisol ambao wanaendelea
kuifanya kuwa kampuni bora zaidi ya sola Afrika Mashariki. Mobisol tunazidi
kuwahakikishia kuwa bidhaa zetu ni bora zaidi na kuna bidhaa mpya zinazidi
kutolewa kila siku kuweza kumlenga kila mwananchi wa Tanzania na tunafurahi
kuona wiki hii tumefikisha wateja 60,000 katika
familia ya Mobisol”Alisema.
Alisema kuwa Mobisol inaendelea kuboresha huduma zake
nchini kwa kupanua mtandao wake wa kuwaunganisha wananchi na nishati ya jua
ikiwemo kuhakikisha wateja wanafurahia matumizi ya nishati hiyo sambamba na
watumuaji wa umeme wa kawaida kutokana na kusambaza pia vifaa bora na imara kwa
matumizi ya nyumbani na biashara kama vile Redio, Mashine za kunyoa, MobiChaja,
tochi pamoja na TV
Rwechungura alisema kuwa mwaka huu Mobisol imepania
kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya nishati ya Jua, kwa maana hadi sasa
tunamuwezesha mteja wetu apate karibu mahitaji yote ambayo angeyapata akiwa na
Umeme wa kawaida. Hatutoi tu sola, bali na vifaa karibu vyote ambavyo ni muhimu
kwa mahitaji ya nyumbani na biashara kama Redio, Mashine za kunyoa, MobiChaja,
tochi pamoja na TV.
Alimalizia kwa kuwakumbusha wateja wote wa Mobisol
kuwa kila mteja anayeshawishi mteja mpya kujiunga na mtandao huo anafaidika kwa
kujipatia kamisheni nono.



0 Comments