Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),
Selemani Jafo akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Manzase wilaya ya
Chamwino alipokuwa anakagua mtambo wa
kusukuma maji kijijini hapo .
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akiangalia
mtambo unaosukuma maji katika kijiji cha
Manzase wilaya ya Chamwino.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akiangalia bomba la
maji ambalo linasambaza maji katika kijiji cha Manzase wilaya ya Chamwino .
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
akiangalia tenki la maji katika mradi wa maji katika kijiji cha Manzase wilaya ya Chamwino .
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa
Manzase aliowakuta wakichota maji.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akikagua tenki la maji
katika kijiji cha Manzase wilaya ya
Chamwino .
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akiwa picha na
wananchi wa kijiji cha Manzase
alipotembelea kukagua mradi wa maji katika kijiji hicho.
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka wananchi wa kijiji
cha Manzase, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kuhakikisha kuwa wanatunza
miundombinu ya mradi wa maji ulioanzishwa kijiji hapo ili uweze kudumu kwa muda
mrefu.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji hicho, katika ziara aliyoifanya ya kukagua mradi wa maji wa kijiji hicho, Jafo alisema
iwapo wananchi hao watautunza mradi huo vizuri utawasaidia kwa kuwa wamepata
taabu ya maji kwa kipindi kirefu.
“Kumekuwa
na kawaida ya baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali ambapo miradi ya
namna hii imekuwa ikianzishwa kwa makusudi kabisa, wanaiharibu miundombinu ya
miradi hii kwa kukata mabomba kwa makusudi
kwa lengo la kunywesha mifugo, kuiba vifaa mbali mbali kwenye mabomba na
kuiba mitambo inayosaidia kusukuma maji” alisisitiza Jafo.
Aidha,
aliwataka Viongozi wote wa kijiji hicho kuhakikisha kuwa kamati ya maji ya
kijiji ambacho ndicho chombo maalumu cha kusimamia maji katika ngazi ya kijiji
kinasimamiwa ipasavyo.
Alisema kumekuwepo
na tabia ya baadhi ya viongozi hao kujimilikisha miradi hiyo kwa kutumia fedha
zinazokusanywa kwa matumizi yao wenyewe, na pindi miundombinu inapoharibika
kijiji kinakosa fedha za kufanya marekebisho.
Naye,
Diwani wa kata ya Manzase Steven Kwanga alisema, mradi huo wa maji
utasaidia sana katika ukuaji wa uchumi wa wananchi wake kwani wamekuwa
wakitumia muda mwingi kutafuta huduma ya maji.
Aidha
alisema wananchi wamekuwa wakitumia kiasi kikubwa cha fedha kununua maji badala
ya fedha hiyo ingetumiwa kutimiza mahitaji mengine.
Jafo alimpongeza
Mbunge wa Jimbo la Mtera ,Livingstone Lusinde kwa kushirikiana na wananchi wake
ambao wiki iliyopita aliambatana nao mpaka viwanja vya Bunge kuonana naye ambapo
Naibu Waziri huyo aliwaelekeza wataalam wa Tamisemi na wataalam wa Halmashauri
ya Chamwino kufanya Manunuzi ya haraka ya Jenerata ili mradi huo uweze kuanza
kazi
Mradi huo
wa maji wa kijiji cha Manzase unatarajiwa kuzinduliwa wakati wowote mwezi huu
kwani mkandarasi wa mradi huo akishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI amekwisha
ukamilisha kwa kiasi kikubwa na unatarajiwa kuhudumia idadi ya watu wasiopungua
8000.








0 Comments