Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na Watendaji wa
Mkoa wa Simiyu wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi
ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Itilima, Bw. Mariano Mwanyigu akitoa maoni wakati wa kikao kazi na Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro
(hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
2017.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akipata
maelezo ya usindikaji maziwa kutoka kwa Mthibiti Ubora wa Halmashauri ya Wilaya
ya Meatu, Bw. Gerald Baruti alipotembelea Kiwanda cha kusindika Maziwa (Meatu
Milk) kilichoanzishwa na vikundi vya vijana kwa kushirikiana na Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiangalia
bustani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, alipotembelea shughuli za maendeleo
za Wilaya ya Meatu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
2017. Kushoto kwake ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,
Bi. Upendo Naftali
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (Wa tatu kulia), akifuatilia
taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (Wa pili kulia) kabla ya kukutana na Watendaji wa
Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias
Kabunduguru.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw.
Antony Mtaka (katikati) akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti
ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia), alipokuwa akizungumza nae
kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.






0 Comments