Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack
Kangese akizungumza na wananchi katika maadhimisho hayo kwenye viwanja vya
shule ya msingi Idukilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga akifurahia jambo na kumpa zawadi mtoto aliyeigiza kama
askari katika maadhimisho hayo.
Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Joseph Swalala akizungumza neon katika maadhimisho hayo.
Sehemu ya watoto wakifuatilia maadhimisho hayo.
Diwani wa kata ya Idukilo palikofanyika maadhimisho
hayo, Sara Michael akizungumza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza.
Watoto wa shule wakiigiza kikao cha Bunge namna
kinavyofanyika.
Kwaya ya watoto wa shule ikiimba wimbo maalumu mble ya
wageni wakati wa maadhimisho.
Sehemu ya watoto wakifuatilia maadhimisho hayo.
Watoto wa shule wakitumbuiza kwa kuimba kwaya.
Watoto wakionesha umahiri wao wa kuimba wimbo wa kufoka
foka ‘Rap’ wenye ujumbe mahsusi.
Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack
Kangese akimpongeza na kumkabidhi zawadi mmoja wa watoto waliofanya vizuri
katika mitihani yake.
Na Robert Hokororo
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga,
Shadrack Kangese leo ameongoza wananchi wilayani humo kuadhimisha kumbukumbu ya
Siku ya Mtoto wa Afrika.
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kata ya Idukilo,
Kangese alisema wazazi wana wajibu wa kuhakikisha wanatengeneza mazingira ya
ulinzi kwa watoto wao badala ya kutegemea Serikali pekee.
Alisema wazazi wanapaswa kubeba jukumu la hakikisha
watoto hawafanyiwi vitendo vya unyanyasaji na kuwa wanapaswa kutoa huduma
muhimu kwao ili waweze kuwa na maendeleo.
Alisema wazazi wanaposhindwa kuwalinda watoto wao
matokeo yake hupata matatizo mbalimbali yakiwemo mimba za utotoni hivyo
hushindwa hukatiza masomo yao.
Aidha katibu tawala huyo wa wilaya hiyo alikemea tabia
ya baadhi ya wazazi wasio waaminifu ambao huwa kikwazo kwa krsi za ukatili
dhidi ya watoto zikiwemo za ubakaji na husa.
Aliwataka kutoa ushahidi kwenye vyombo vya usalama pindi
watoto wao wanapotendewa ukatili badala ya kukaa kimya kwa maelewano na
wanaowafanyia vitendo hivyo.
“Kila siku watoto wetu wanatendewa vitendo vya ukatili
vikwemo ubakaji, utekwaji na hivyo hupunguza muda wa kuishi shule zinawajibika
kutengeneza mazingira mazuri ya waoto ili wasipopatwe na matatizo haya,”
alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga aliwataka wazazi wote kuhakikisha watoto wao
wanahudhuria shuleni.
Magoiga alisema kuwa kama watoto hawaendi shuleni kwa
mujibu wa utaratibu haki ya kupata elimu waliyonayo haitakuwa na maana kwani
wanakuwa wanakosa masomo.
Alisisitiza kuwa vipaumbele vyake ni vitatu ikiwemo
elimu na kuwa katika moja ya huduma ambazo halmashauri inatekeleza kwa wananchi
ni elimu kwa watoto wote.
Mkurugenzi mtendaji huyo aliwataka watoto wa kike
wasidanganywe bali watumie nafasi waliyo nayo kusoma kwa bidii na kufaulu ili
kufikia malengo yao.
Kaulimbi kwa Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka huu ni Maendeleo
endelevu 2030: Imarisha ulinzi na haki sawa kwa watoto
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa duniani kwa lengo
la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani na maadhimisho haya
hufanywa kila Juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na Umoja
wa Afrika (EU).













0 Comments