Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa kutoka
kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala ya kikosi kazi cha mkoa wa
Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya
Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala wakati wa
uwasilishwaji wa taarifa ya
kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka
kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali
na Chunya
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza mbele Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala pamoja na kikosi kazi chake wakati wa
uwasilishwaji wa taarifa ya
kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka
kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali
na Chunya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala
pamoja na kikosi kazi chakemara baada ya kupokea taarifa ya
kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka
kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali
na Chunya .
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza
Wakuu wa wilaya nchini kuchukua hatua stahiki katika kulinda na kuhifadhi
mazingira katika wilaya zao ili kukabiliana uharibifu mkubwa wa mazingira kwenye
misitu na vyanzo vya maji ili visikauke na kuleta athari kwa binadamu na viumbe
wengine.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mara baada ya kukabidhiwa Taarifa
ya Kikosi Kazi cha Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa mkoa wa huo Amos Makalla kuhusu
Mapendekezo ya Marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji
katika wilaya za Mbarari na Chunya - Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la uharibifu wa mazingira katika
baadhi ya wilaya nchini ni kubwa hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa Wakuu wa wilaya kwa
ushirikiano na watendaji wengine katika kukabiliana na hali hiyo kwenye maeneo
yao.
Amesema kabla
ya hatua kuchukuliwa ni vizuri wananchi wakaelimishwa kuhusu umuhimu wa
uhifadhi wa mazingira kabla ya kuondolewa kwenye maeneo waliyovamia ikiwemo
maeneo ya vyanzo vya maji.
Makamu wa
Rais pia amepongeza timu ya wataalamu wa kikosi kazi cha Mkoa wa Mbeya kwa kazi
kubwa na nzuri waliyoifanya inayolenga kuokoa mfumo wa ikolojia katika Bonde la
Mto Ruaha Mkuu.
Kwa upande
wake, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amemweleza Makamu wa Rais kuwa aliamua
kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa mpaka kati ya
wananchi wa wilaya ya Chunya na Mbarali na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, uharibifu
wa mazingira na upotevu wa maji kwenye Mto Ruaha Mkuu.
Mkuu wa mkoa
wa Mbeya Amos Makalla baada ya kukabidhi taarifa ya kikosi kazi kwa Makamu wa
Rais amesema kikosi kazi hicho kimependekeza vijiji Tisa kati ya 33 ambavyo
vina mgogoro na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha viondolewe kabisa kwenye eneo la
hifadhi na vijiji vingine Vinne vinatakiwa kufutwa na wananchi kuhamishwa
kwenye maeneo hayo na Serikali itawalipa fidia na kuratibu eneo
watakapohamishiwa.






0 Comments