Baadhi ya wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiaga mwili wa marehemu Francis Maige Kanyasu (86) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo na wakati akiendelea na matibabu mauti yakamkuta.
Baadhi ya watu waliofika wakiuaga mwili huo leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Muhimbili wakisubiri kuuaga mwili huo leo. Kulia ni Zuhura Mawona ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Uuguzi, Agness Mtawa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi.
Mkurugenzi wa Huduma na Upasuaji wa Muhimbili, Dk Julieth Magandi akiwashukuru watu mbalimbali walofika kuuaga mwili huo leo.
Mkurugenzi wa Huduma na Upasuaji wa Muhimbili, Dk Julieth Magandi akiwashukuru watu mbalimbali walofika kuuaga mwili huo leo.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dk Juma Mfinanga akieleza jinsi Hospitali ya Muhimbili ilivyokuwa ikimpatia matibabu mzee Francis Maige Kanyasu.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulusubisya akizungumza kabla ya shughuli za kuaga mwili huo leo.
Mwili wa
marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu
umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kusafirishwa na serikali kwenda kijijini
kwao Igokero wilayani Misungwi.
Shughuli ya
kuuaga mwili huo imeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya
Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel
Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Mpoki
Ulusubisya.
Akizungumza
katika shughuli hiyo Bwana Katemba ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
jitihada kubwa walizofanya za kumpatia tiba na kumuhudumia kwa kipindi
alichokuwa amelazwa hospitalini hapo.
“Nawapongeza
Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu, lakini
kazi ya Mungu haina makosa , pia sina budi kuwashukuru majirani zake na uongozi
wa Serikali ya Mtaa wa Malapa kwa kujitoa naomba mfanye hivyo hata kwa wazee
wengine’’ amesema Katemba.
Naye Mkuu wa
Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk. Juma Mfinanga amesema walimpokea
Mzee Kanyasu Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana alikokua akipatiwa
matibabu na walipomfanyia vipimo vya awali waligundua kwamba ana maradhI ya
Kifua Kikuu ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu kutokana na mazingira aliyokua
akiishi.
Hivyo Dk.
Juma ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kwenda hospitalini mapema pindi
mtu anapoona hali yake ya kiafya si nzuri kwani ukiwahi hospitali ni rahisi kupata
tiba na kupona kuliko kusubiri hadi
ugonjwa uwe sugu.
Mzee Francis
Maige Kanyasu alizaliwa 1931 na kufariki dunia Mei 29 , 2017 saa mbili na nusu
usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.










0 Comments