Wakati mshambuliaji Ibrahim Ajib
akiwa anaelekea Jangwani, klabu ya Simba inaonekana kutokuwa na shida
juu ya hilo kwasababu tayari ipo njiani kumvalisha Emannuel Okwi Jezi 25
msimu ujao.
ambaye ameshaitumikia Simba kwa
vipindi viwili tofauti, ametua Bongo jana usiku na leo mchana nilipata
nafasi ya kuzungumza na amethibitisha kwamba yupo katika mazungumzo ya
mwisho ya kujiunga na Simba.
“Ni kweli nipo kwenye mazungumzo
ya mwisho na Simba, naamini tutakubaliana kila jambo na nitasaini
kuichezea tena Simba.” – alisema Okwi.
Tayari mwenyekiti wa kamati ya
Usajili wa timu ya Simba Zacharia Hans Poppe ametua nchini Uganda
kunamalizana na mchezaji huyu ambaye anacheza timu ya AS Villa
Updates: Muda mfupi uliopita, klabu ya Simba kupitia msemaji wao
Haji Manara wamethibitsha Okwi amemwaga wino wa kuitumikia Simba,
mkatabawa miaka miwili.

0 Comments