KAMISHNA Panga, akikabidhi
zawadi wa Sister Stella Selugenge wa Makao ya Yatima Msimbazi, Dar es Salaam.
KAMISHNA Panga, akikabidi
zawadi kwa Ofisa Ustawi wa Jamii Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Yatima
Kurasini, Dar es Salaam, Beatrice Mgumiro.
KAMISHNA Msaidizi katika
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Simon Panga,
akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi ya Idd El Fitri kwa niaba ya Rais Dk.
John Magufuli kwaVituo vya Yatima na Makundi Maalumu katika Maabusu ya Watoto
Dar es Salaam, leo.
Na. Lilian Lundo -
MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi ya Idd El
Fitri zenye thamani ya shilingi 10,922,000 kwa vituo 9 vya Mkoa wa Dar es
Salaam, vituo 2 vya Zanzibar na vituo 13 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.
Zawadi hizo zimekabidhiwa
leo katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga Jijini
Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Idara ya Ustawi wa
Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Simon Panga
kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Panga amezitaja
zawadi zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo
zitawezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu
wengi.
“Mhe.
Rais kwa upendo
wake wa dhati kabisa ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio
katika
makundi maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na
wazee wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa katika makazi, katika
kusherehekea sikukuu ya
Idd El Fitri mwaka 2017,” amesema Panga.
Aidha, amevitaja
vituo vilivyonufaika na zawadi za Mhe. Rais kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Makao
ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto IBN Kathry- Ilala,
Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Makao ya Watoto Yatima Chakuwama, Makao ya
Watoto Yatima Group Trust Fund – Temeke, Makao ya Watoto Yatima Dar Al Arqum
(International Islamic Relief Organization), Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam –
Upanga, Makazi ya Wazee na Wasojiweza Nunge – Kigamboni na Shule ya Ufundi ya
Watoto Wenye Ulemavu Yombo.
Vile vile, amevitaja
vituo vilivyonufaika kwa upande wa mikoa ya Tanzania Bara kuwa ni Makao ya
Watoto Tosamaganga – Iringa, Makao ya Watoto Yatima Malaika Kids Home, Mkuranga
– Pwani, Makao ya Watoto Yatima Karibu
Nyumbani, Kibaha – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Miyuji Cheshire – Dodoma,
Shule ya Maadilisho Irambo – Mbeya na Mahabusu ya Watoto – Mbeya.
Vituo vingine ni
Mahabusu ya Watoto – Arusha, Makao ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto –
Sinyanga, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ngehe – Ruvuma, Makazi ya Wazee na
Wasiojiweza Kiilima – Bukoba, Kagera, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Magugu –
Manyara, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ipuli – Tabora, Makazi ya Wazee na
Wasiojiweza Bukumbi – Mwanza.
Kwa upande wa
Zanzibar, vituo vilivyonufaika ni Kituo cha Watoto Yatima Mabaoni – Chakechake
– Pemba na Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Sebleni – Unguja.
Utoaji wa zawadi hizo
ni utaratibu wa Waheshimiwa Marais tangu awamu nne zilizopita ambapo wamekuuwa
wakiwapatia makundi hayo maalum zawadi za vyakula katika sikukuu mbalimbali.




0 Comments