
Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akipeana mkono na mwenyekiti,
Boniface Butondo baada ya kupokea cheti kwa ajili halmashauri yake kufanya
vizuri katika upandaji miti.

Mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya Kishapu, Boniface Butondo akizungumza wakati wa sherehe hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Talaba akiangalia alizeti kwenye banda la Halmashauri ya wilaya hiyo
wakati wa sherehe hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Talaba akiwa na viongozi wengine wakimsikiliza mtalaamu kuhusu
majiko yasiyotumia kuni wakati akitembelea mabanda.
Ofisa Kilimo kata ya Ngofila,
Genes Tarimo (kushoto) akiwapa maelezo kuhusu madumu maalumu vya kuchemshia
maji ya kunywa mgeni rasmi na viongozi aliombatana nao.
Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (kulia) na Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga, Josphine Matiro (kushoto) wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa
Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi (katikati).
Ofisa kutoka Mgodi wa
Williamson Mwadui akitoa maelezo kwa wageni kuhusu jiko linalotumia sola
kupikia vyakula mbalimbali bila kutumia kuni wala mkaa.
Sehemu ya vitalu vya miche
vikiwa katika banda la maonesho vikiwa tayari kwa ajili ya kuonesha wananchi
namna ya kupandwa.
Wananchi wakitembelea
banda la halamashauri ya wilaya ya Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,
Nyabaganga Talaba (wa pili kushoto) akionesha furaha yake kwa kuserebuka na
kwaya ya wanafunzi.
Mgeni rasmi, Mkuu wa
wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akipata maelezo kutoka banda la mgodi wa
Williamson Mwadui. Nyuma yake ni mkurugenzi mtendajihalmashauri ya wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ametumia Siku
ya Mazingira Duniani kuwaagiza viongozi katika ngazi mbalimbali kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu athari zinazotokana na vitendo vya ukataji miti.
Ametoa agizo hilo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake
na Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba leo wakati wa kilele cha siku hoyo
kilichofanyika kimkoa kata ya Mwamashele wilayani hapa.
Alisema kuwa wananchi wengi hawaelewi kuwa tunapokata
miti kwa wingi tunatishia uhai wetu na wa wanyama hali inayotokana na ukosefu
wa mvua na hivyo kusababisha ukame.
Telack alisema kuwa misitu ndiyo mhimili mkubwa wa
kulinda mazingira yetu na kutupatia nishati, dawa za asili, vifaa vya ujenzi
pamoja na kuboresha hali ya hewa.
“Pamoja na muhimu wa misitu kwa binadamu na mazingira
imekumbwa na uharibifu mkubwa katika mkoa wetu wa Shinyanga kwa matumizi
mbalimbali yakiwemo ya uchomaji mkaa,” alisema.
Aliongeza kuwa uchomaji wa mkaa katika maeneo mengi kama
vile Nyasamba umekuwa kama shughuli ya kujipatia kipato na hivyo kutishia
kutoweka kwa misitu.
Aliwataka wadau kutumia nishati mbadala kama vile
vinyeshi vya wanyama na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi hayo kwani matumizi
ya mkaa ni adui wa mazingira.
Mkuu huyo wa mkoa alionya kuwa uchomaji mkaa na utumiaji
wake huongeza hewa ya ukaa na kusababisha mabadiliko ya tabia ya nchi na
hatimaye kuleta ukame.
“Hivyo ni vema wananchi tubadilike
na tuachane na matumizi ya rasilimali zetu kuwa endelevu kwa kupanda miti zaidi
ili tuhifadhi ardhi, vyanzo vya maji na kuboresha hali ya hewa,” alisema.
Sherehe hizo zilihudhuriwa
pia na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine
Matiro, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniface Butondo,
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga,
wakurugenzi wa halmashauri za Ushetu, Msalala, Shinyanga na Kahama.
Sherehe hizo ambazo
kitaifa zilifanyika jana mkoani Mara zinachagizwa na kaulimbiu ya Hifadhi ya
Mazingira ni muhimili kwa Tanzania ya Viwanda.











0 Comments