Na, Twaha Twaibu
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ni
mamlaka iliyoanzishwa kwa Amri ya Serikali na kutangazwa kwenye gazeti la
Serikali Na.135 la tarehe 9 Mei, 2014. Uanzishwaji wa Mamlaka hii ni
utekelezaji wa kifungu cha 8 cha Sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka
2009.
Mamlaka ya Wanyamapori imeanza
kazi rasmi tarehe 1/Julai/2016. Makao makuu yake kwa sasa yapo Morogoro katika
jengo la Taasisi ya utafiti wa mazao ya misitu (TAFORI). Majukumu ya TAWA ni
kusimamia na kulinda wanyamapori wote waliyopo maeneo ya nje za Hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongororo.
Picha ya pamoja kati ya Katibu Mkuu na Walimu wa mafuzo hayo kutoka
Marekani waliyochuchuma.
Wizara ya
Maliasili kupitia Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imetoa mafunzo ya kijeshi ya kukabiliana na
Ujangili wa wanyamapori kwa Askari wanyamapori wapatao 75 kutoka katika Mapori
ya Akiba Rungwa, Ugala na vikosi Dhidi ya ujangili vya Manyoni na Arusha.
Mafunzo
hayo yalifanyika katika Pori la Akiba
Rungwa/Muhesi/Kizigo, yakiendeshwa na askari wa jeshi la Marekani. Mgeni rasmi
alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mej.Generali Gaudence S.
Milanzi akifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa
TAWA Bw. Martin Laibooki, Mkurugenzi
uzuiaji ujangili wa TAWA Bw. Faustin Masalu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
wanyamapori Bw. Canisius Karamaga, muwakilishi wa ubalozi wa Marekani ambaye ni
Mwambata wa jeshi la Marekani hapa nchini Tanzania Liutenat Colonel Michael
Lee, na wawakilishi wa mashirika ya wafadhili wa mafunzo hayo wawili kutoka
mashirika tofauti, Bw. Aaron Nicholas toka Shirika la ‘ Wildlife Conseration
Society- WCS) na Bw. Trevor Johnes toka shirika la uhifadhi la ‘STEP’. Aidha kulikuwa na wawakilishi wengine kutoka
mkoa wa Singida wakiwepo muwakilishi wa
RC na RPC.
Picha ya pamoja Katibu Mkuu
na wahitimu Askari wanyamapori. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi amewataka wahitimu wa mafunzo hayo waliyopata kukabiliana na vitendo vya ujangili kwa kuwakamata majangili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
alitoa nasaha hizo wakati akifunga mafunzo ya watumishi wa wizara , Aidha alishuhudia mafunzo ya vitendo yalitoendeshwa kwenye makao makuu ya Pori la Rungwa kama picha hapo chini zinzvyoonyesha.
Doria inaendelea na hatimaye jangili amekamatwa na kujeruhiwa baada ya mashambulizi makali na kubebwa kusudi apate huduma ya kwanza.
Mafunzo
hayo yalianza Machi 27 hadi Juni 5, mwaka huu 2017 kwa maofisa 75 . Mafunzo
waliyojifunza yalijikita kwa masomo yafuatayo; Upelelezi, Huduma ya
kwanza,mbinu za kufanya doria, mazoezi ya viungo,usomaji wa ramani, GPS,
ushirikishaji jamii katika uhifadhi na matumizi ya siraha.
Katika
kushirikiana na Serikali ya Marekani kupitia mashirika ya WCS na STEP
wamesaidia vifaa mbalimbali katika
Mapori ya Akiba ya Rungwa/Muhesi/Kizigo vifaa hivyo ni pamoja na magari manne, tractors
2, mafuta ya magari.
Afisa wanyamapori Bw.Baraka Baragae akielezea vitendo vya mafunzo
vinavyoendelea hapo chini na jangili amekamatwa.
| Jangili amekamatwa. |
Katibu Mkuu aliwaeleza wahitimu kuwa,yeye binafsi
natambua kuwa mafunzo haya hayakuwa rahisi kwenu haswa ukizingatia wengi wenu
kama siyo wote, hii ndiyo mara yenu ya kwanza kupata mafunzo kama haya,lakini
kwa dhamira nzuri na yenye mtazamo chanya mliyokuwa nayo imepelekea wote
kumaliza salama.
Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatasaidia kuimarisha
nidhamu kwenye maeneo yetu ya kazi
katika kipindi hiki tunachojianda kuingia katika mfumo wa kiutendaji wa jeshi
usu.
Katibu Mkuu aliwaeleza wahitimu kuwa Wizara inatambua
mchango wa TAWA tangu kuanzishwa katika kukabiliana na ujangili. Kuanzia mwezi
Julai 2016 jumla ya majangili 3,185 wamekamatwa, kati ya hao 1539 wamefikishwa
mahakamani, na siraha 270 na risasi 1058
zimekamatwa. Aidha askari wametegua mitego 3,273 ya kuua wanyamapori. Nawapongeza
sana TAWA.
Alimalizia hotuba yake kwa kuipongeza Serikali ya
Marekani na Mashirika yasiyo ya kiserikali ya WCS na STEP kwa mchango wake
katika uhifadhi.
Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw.Martin Loibooki alimueleza
mgeni rasmi kuwa Katibu lengo kubwa la
mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kuongoza watumishi walio chini yao ambao
wengi ni askari.wakati wahitimu hawa wengi wao hawajapata mafunzo ya kijeshi
tangu wamalize elimu yao ya chuo kikuu. Bw.loibooki alisema majukumu waliyopewa
ni makubwa ambayo lengo lake ni kuwaanda kuwa wahifadhi wakuu na baadaye. Hivyo
ni vyema wakatambua kuwa baada ya mafunzo haya wanajukumu yanawasubiri mbele
yao.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw. Martin T.Loibooki, alianza hotuba yake kwa
kumshukuru Katibu Mkuu kukubali kuja kufunga mafunzo hayo ya Maafisa wanyampori
Bw.loibooki alielezea kidogo Mamlaka anayoisimamia kwa
kuanza kusema, Mamlaka ilianzishwa na Serikali kama chombo cha utekelezaji wa
majukumu ya Serikali kwa niaba ya Serikali chini ya uangalizi wa Serikali
na kuwa na mfumo unaonesha utekelezaji
wa majukumu kwa ufanisi zaidi.
Kama ilivyo kwa Mamlaka Serikali nyingine
nchini, lengo la kuanzishwa TAWA ni kutekeleza majukumu ya Idara ya Wanyamapori
hasa ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini. Majukumu ya
TAWA ni kusimamia shughuli za utawala, ulinzi, usimamizi wa raslimali ya
Wanyamapori katika maeneo yote nje ya Hifdahi za Taifa na Hifadhi ya Ngorongoro.
Akiitimisha hotuba yake Bw. Loibooki alizungumzia
suala la ujangili kwa kusema, TAWA inaamini kwamba changamomoto za ujangili na
uvunaji haramu wa misitu na matatizo mbalimbali yanayohikabili uhifadhi nchini
hayawezi kutatuliwa kwa mfumo wa utendaji kazi wa kiraia. Hivyo, Wizara
inakamilisha taratibu za kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka wa kiraia
kwenda jeshi usu.Mabadiliko haya ya kimfumo ni matakwa ya Sheria ya Uhifadhi
Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009 ambayo imeanisha kwamba kutaundwa kikosi cha
jeshi usu (Wildlife Protection Unit),
ili kuhakikisha ulinzi kamili wa rasilimali katika maeneo yaliyohifadhiwa
WAHITIMU WA MAFUNZO WANASOMA RISALA KWA MGENI RASMI WAKISHUHUDIWA NA MC.
Bw.
Loibooki alimueleza mgeni rasmi anawashukuru Serikali ya Marekani kupitia
shirika lisilo la Kiserikali la WCS kwa kutoa mafunzo ya kikosi maalumu cha
kukabiliana na ujangili kwa haraka zaidi kiitwacho ‘Rapid Response Team’
ambacho kimepatiwa vifaa ikiwepo magari ya doria kwenye Mapori ya Akiba ya
Rungwa, Rukwa na Piti. WCS vilevile wanasaidia doria ya kutumia ndege katika
kukabiliana na ujangili.Hapo chini ni baadhi ya kikosi hicho.
KAIMU MKURUGENZI MKUU BW.LOIBOOKI AKITELEMKA KWENYE UWANJA WA RUNGWA AKIWA AMEFUATANA NA KATIBU MKUU. KATIBU MKUU AKISALIMIANA MA MKUFUNZI WA MGAMBO WILAYA YA MANYONI BW. Lala Awe Silago.
Katibu Mkuu akisalimiana na Mratibu wa shirika la STEP Bw.Travor Johnes.
Katibu Mkuu Mej.General. Gaudence Milanzi akisalimia na mwambata wa jeshi la Marekani nchini Tanzania Liutenant Colonel Micheel Lee kwenye Pori la Rungwa.
Katibu Mkuu akisalimiana na Mratibu wa Shirika la WCS Bw. Aaron.
Katibu mkuu akisaini kitabu cha wageni ndani ya Ofisi ya Makao makuu ya Pori la Rungwa, pembeni ni meneja wa Pori Bw. Saidi Kabanda.
KATIBU MKUU AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAHITIMU . |

0 Comments