Baadhi ya wakazi wa Mangwi Mchukwi wilaya ya Kibiti ,wakiwa msibani (picha na Mwamvua Mwinyi)
Muenezi wa CCM Rufiji ,Musa Mnyelesa aliyeshika mtoto ,akiwa amekwenda kuifariji familia ya marehemu Shamte ambae alikuwa ni mtendaji wa kijiji cha Mangwi ,Mchukwi ambae aliuawa na nyumba yake pia ilichomwa moto (picha na Mwamvua Mwinyi )
Nyumba zilizochomwa moto kwenye tukio la mauaji yaliyotokea usiku wa kuamkia June 28 huko Kibiti .
Na
Mwamvua Mwinyi ,Pwani
BAADHI
ya wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM)wilayani Kibiti na Rufiji,mkoani Pwani
,wameutaka uongozi wa CCM Taifa kuangalia namna ya kuahirisha uchaguzi wa chama
kwenye wilaya hizo ama mkoa kijumla .
Wameeleza
hatua hiyo itawezesha wanachama kujipanga kwa wakati mwingine ili kupisha
kadhia ya mpito ya vitendo vya mauaji vinavyoendelea .
Aidha
wamesema vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendeleo na uchumi wilayani humo na
kukwamisha mipango ya kikanuni na taratibu za vyama walizojipangia .
Hata
hivyo ,wamesisitiza uwezekano wa vyama vya siasa vikubwa wilayani hapo, kukaa
kwa pamoja na wazee wa pande zote kukemea vitendo hivyo.
Wakazi
hao walibainisha kwamba,kwa umoja wao kutawezesha kushirikiana na serikali
kumaliza janga hilo.
Muenezi
wa Ccm wilaya ya Rufiji ,Musa Mnyelesa ,mkazi wa Kibiti Hadija Issa ,Hamis
Kidongezo na Seif Mohammed waliyasema hayo,baada ya kutokea mauaji ya
mwenyekiti wa kijiji na mtendaji Wa kijiji cha Mangwi ,Mchukwi usiku wa kuamkia
June 28 .
Walieleza
,hadi sasa hakuna uchaguzi uliofanyika wa ngazi za chini ambako maeneo mengine
unafanyika ,hakuna anaechukua fomu ya kugombea .
Wanaongeza
kuwa kila mwanachama anahaki ya kugombea na kupiga kura ili kuimarisha chama
chochote kile .
Walisema
kutokana na vitendo vinavyotia shaka na kuonyesha Kibiti na Rufiji kutokuwa
shwari ,ni vyema uchaguzi ukaahirishwa ili baadae kupata haki za kichama wakiwa
na amani .
Muenezi
wa CCM Rufiji ,alisema chama mkoa na taifa wanapaswa kutupia macho suala hilo
kwa upana kwa maslahi ya chama .
Mnyelesa
alisema serikali na askari polisi wanafanyakazi nzuri lakini inabidi kujulikane
kina cha tatizo.
"Naona
kuna haja ya vyama vyote vikaguswa na hili ,maana hii agenda lisingekuwepo
bunge ina maana viongozi wa vya vingine vinavyokuwa na sauti kubwa ya kutetea
mengi wasingeongeaa"
"Tunaomba
wanasiasa ,viongozi wa dini ,wanaharakati washikane mkono kuongeza juhudi za
kupiga kelele kwa hili kama ilivyo katika mambo mengine ya kijamii
wanavyofanya" alisema Mnyelesa.
Mnyelesa
alielezea kwamba ,bado wananchi ambao ni wanachama na viongozi wa CCM,
vitongoji na vijiji wanaishi kwa hofu .
Nae
Seif, alisema baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji wanashindwa kwenda
ofisini kutekeleza majukumu yao.
Alisema
wanaishi kwa sintofahamu na imani inawatoweka.
Anaeleza
miaka ya nyuma watu walikuwa wakigombea nafasi mbalimbali za uongozi lakini kwa
sasa wanakwepa na kuhofia uhai wao,na anahofu hata u
chaguzi wa serikali za
mitaa 2019 kuwa wengi hawatajitokeza.
Hadija
aliiomba serikali kuwadhibiti wahamiaji haramu kwa kuwarudisha makwao badala ya
kuachiwa kwani yawezekana wakaleta athari kubwa ndani ya Mkoa na taifa kijumla
.
Hadija
alisema pia tatizo la wafugaji na wakulima liangaliwe kwani isije ikawa
linachangia.
Nae
mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo, aliwaomba wananchi washirikiane
na serikali kuwafichua wahalifu .
Ndikilo
,alieleza wauaji ama wahalifu wapo ndani ya jamii hivyo endapo wananchi
wataamua kuwataja watu hao itawasaidia kuwakamata kirahisi.
Mkuu
huyo wa Mkoa ,aliwataka kuwasema pia wageni kwenye maeneo yao kwani wageni
wengine sio watu wema.
Kamanda
wa polisi mkoani Pwani,Onesmo Lyanga alibainisha kwamba,wanaendelea kupambana
na kuimarisha ulinzi .
Ni
matukio takriban 37 ya mauaji ya viongozi mbalimbali wa chama, wenyeviti
wa vijiji /vitongoji na askari polisi ambayo yanadaiwa kujitokeza wilayani
Rufiji ,Mkuranga na Kibiti,tangu mwaka 2015.
Katika
matukio hayo ni pamoja la March 28 ambapo mwenyekiti wa (CCM) tawi la
Mparange na mjumbe wa serikali ya kijiji cha Ikwiriri Kaskazini ,Michael
Lukanda,aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwani .
Jingine
ni march 12,mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo Hemed Njiwa aliuawa kwa
kupigwa risasi.
Jan
19,mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa
kupigwa risasi.
March
1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana aliuawa.
Feb
24,watu watatu akiwemo afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Kibiti Peter Kubezya
aliuawa kwa risasi.
April 13 mwaka
huu,yalitokea mauaji ya askari polisi nane waliouawa kwa kupigwa risasi na
wahalifu waliokuwa na silaha za moto .
Octoba
24,2016 afisa mtendaji wa kijiji cha Nyambunda Ally Milandu alipigwa risasi na
kufa.
Novemba
6,2016 ,mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang'unda kijiji cha Nyambunda Mohammed
Thabiti alipigwa risasi akielekea kwake.
Matukio
mengine ni sanjali na May 17 ,mwenyekiti wa CCM tawi la Njianne ,kijiji cha
Muyuyu ,ambae pia ni mjumbe wa kamati ya siasa kata ya Mtunda ,Iddi Kilungi ,aliuawa
kwa kupigwa risasi.
May
13 mwaka huu,katibu wa CCM kata ya Bungu ,wilayani humo,Halife Mtulia ,kuuawa
kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
June
28 mwaka 2017 ,mtendaji wa kijiji cha Mangwi,Shamte Makawa na mwenyekiti wa
kijiji ,Hamis Mkima waliuawa na nyumba tatu kuchomwa moto.
Na june 21 mwaka
huu,askari Polisi wawili wa kikosi cha usalama wa Barabarani wilayani Kibiti
,waligwa risasi na watu wasiojulikana katika kijiji cha Msafiri .




0 Comments