Afisa Mwandamizi wa Tathmini ya Mikopo wa TADB, Bw. Mubezi Buberwa (kulia) akitoa maelezo kuhusu huduma za mikopo inayotolewa na Benki hiyo kwa Waziri mwenye dhamana ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba.
Na Mwandishi wetu, Bukoba
Waziri
mwenye dhamana ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba
ameiagiza Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuharakisha
kutoa mikopo kwa wasindikaji wa maziwa nchi
ili kuongeza tija kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa nchini.
Waziri
Dkt. Tizeba alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Benki
hiyo katika Kilele cha Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa
iliyokuwa ikifanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani
Kagera tangu tarehe 28 Mei na kufikia kilele chake tarehe 01 Juni,
2017.
Dkt.
Tizeba alisema utoaji wa mikopo kwa wasindikaji una umuhimu wa kipekee
kwa kuwa utachangia uhakika wa masoko kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa
nchini hali itakayochochea tija kwa wafugaji
hao hivyo kuchagiza lengo la Serikali la Awamu ya Tano ya kuwawezesha
wakulima, wafugaji na wavuvi kuweza kunufaika na sekta hizo.
“Serikali
ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi
hivyo uanzishwaji wa Benki ya Kilimo lazima usaidie katika kuhakikisha
wasindikaji wa maziwa wanapata huduma
za TADB kwa wakati ili tupate uhakika wa masoko kwa wafugaji wetu ili
tuiinue Tasnia ya Maziwa ili ichangie ukuaji wa uchumi na maendeleo
nchini,” alisema.
Kwa mujibu wa mpango kazi wa TADB,
sekta
ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa
ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika
uongezaji
wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa nchini. Na Benki
imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa
Nyama na Maziwa ili kuongeza tija kwenye Tasnia za nyama na maziwa ili
kuchagiza maendeleo katika tasnia hizo.
Katika
kuhakikisha wasindikaji wa maziwa wananufaika na huduma za TADB, Benki
hiyo inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi
Miaka Miwili
(2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5))
na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano
(15)).
Kwa mujibu wa Mpango Kazi huo, mikopo hiyo ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi
ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
TADB
ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu
mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo
nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi
kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye
upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo;
mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali
halisi ya sekta ya kilimo
na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.



0 Comments