Wizara
ya Maliasili na Utalii inawakaribisha
wananchi wote kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar–es-Salaam (SabaSaba) yatakayofanyika
kwenye Viwanja vya SabaSaba Barabara ya Kilwa kuanzia tarehe 28 Juni
hadi 8 Julai 2017. Karibu ujionee shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya
Maliasili na Utalii.
Wizara
ya Maliasili na Utalii inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa katika Maonesho
ya mwaka huu kutakuwa na kiingilio kwa wale watakaopenda kutembelea Bustani ya
wanyamapori.
Kiwango
cha tozo kitakuwa shilingi 1,000/= kwa watu wazima na shilingi 500/=
kwa watoto. Watoto walio chini ya miaka
mitano wataingia bure. Gharama hizo za viingilio ni kwa ajili ya kuchangia
gharama za utunzaji wa Wanyamapori hai katika kipindi cha maonesho.
Karibu
utembelee Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ujionee wanyamapori hai kama
vile Simba, Chui, Nyati, na ndege wa aina mbalimbali katika mazingira ya kuvutia.
“Njoo ujionee
Wanyamapori hai kukuza Utalii wa ndani”
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
Wizara ya Maliasili na Utalii
S.L.P 1315
Dodoma

0 Comments