Mkuu wa Kampuni ya
mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khatib Baucha (kushoto) akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mifuko ya Saruji kwa
kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi
la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel
walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13
milioni.
Mkuu wa Kampuni ya
mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (kushoto) akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mabati kwa kwa ajili
ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la
makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo
Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh.
13 milioni.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akizungumza na wakuu wa wilaya za mkoa huo Mhe.
Salama Mbarouk Khatib wa wilaya ya ChakeChake (kushoto) na Hemed Suleiman
Abdallah wa wilaya ya Mkoani( wa pili kushoto) kabla ya kuwakabidhi msaada wa
Saruji na Mabati yaliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya
waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo
lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji
mifuko 350 yalikabidhiwa na Kampuni ya Zantel.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akiwakabidhi wakuu wa wilaya wa mkoa huo mabati
yalitolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa
mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo lilifanyika jana
kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 kwa
pamoja vilitolewa na Kampuni hiyo. (Katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya
Chakechake Mhe. Salama Mbarouk Khatib na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkoani
Mhe. Hemed Suleiman Abdallah.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kusini
Pemba, Ndg. Yussuf Mohammed Ali (kushoto) akimtambulisha Mkuu wa
Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (wa pili kushoto) kwa Mkuu wa Mkoa
wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah (hayupo pichani) kabla ya Mkuu
huyo wa Zantel kukabidhi msaada wa Saruji na Mabati kwa ajili ya waathirika wa
mafuriko mkoani humo. Msaada huo una gharama ya Sh 13 milioni na lilifanyika
jana kisiwani Pemba-Zanzibar. Wa tatu Kulia ni Ofisa wa fedha na Utawala wa
Tawi la Zantel–Pemba, Yakoub Fadhil Juma.






0 Comments