Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
akikagua mashine ya EFD na risiti ya kieletroniki aliyopewa baada ya
kununua bidhaa kwenye moja ya maduka mjini Dodoma, alipofanya ziara ya
kushitukiza kukagua kama wafanyabiashara wa mji huo wanatumia ipasavyo
mashine hizo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
akipitia kwa makini fomu ya makadirio ya kodi iliyotolewa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) katika moja ya duka la vipodozi mjini Dodoma
wakati alipofanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD’s katika baadhi
ya maduka yaliyopo mjini humo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
akimuonya mfanyabishara wa mjini Dodoma, Bw. Isdori Shirima, baada ya
kukuta akiuza bidhaa bila kutoa risiti za kielektroniki kwa wateja wake
inavyotakiwa na kuagiza Mamlaka ya Mapato mkoani humo kufanya ukaguzi wa
kina ili kubaini kiwango cha ukwepaji kodi cha mfanyabiashara huyo na
kumchukulia hatua za kisheria.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
akimuagiza Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani
Dodoma, Bw. Ngaka Magere, kumkutanisha na mawakala wanaosambaza mashine
za kieletroniki za kutolea risiti mkoani humo baada ya kutoridhishwa na
huduma zao
Mfanyabiashara wa duka la rejareja mjini Dodoma, Bw. Donald
Chami, akimwonesha mashine ya kieletroniki ambayo imeharibika, Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), baada ya kufanyaziara ya
kushitukiza kwenye duka lake na kubaini kuwa hatoi risiti za
kielektroniki kwa wateja wake.
Kiongozi wa Timu Maalumu ya Ukaguzi wa Mashine za EFD’s kutoka
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Godfrey Patrick (wa
pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kushitukiza
iliyofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb),
kwenye maduka mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
akimwelekeza mwananke mmoja aliyemkuta dukani akague risiti yake baada
ya kufanya manunuzi kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi mjini Dodoma,
alipofanyaziara ya kushitukiza ili kubaini namna wafanyabiashara wa
maduka mjini humo wanavyotumia mashine za kielektroniki za kutolea
risiti.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
akikagua risiti na kupata maelezo kutoka kwa mhudumu wa Kituo cha Mafuta
cha ORYX mjini Dodoma, Bi. Hanifa Shaldin, alipofanya ziara ya
kushitukiza kuangalia kama vituo vya mafuta mjini humo vimefungwa
mashine za kielektroniki za kutolea risiti kwa wateja wao.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akisikiliza
maelezo ya matumizi ya mashine za kielektroniki kutoka kwa mfanyakazi
wa Kituo kimoja cha Mafuta mjini Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza
kituoni hapo kuangalia matumizi ya mashine hizo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb)
(katikati) akiwa na katika mitaa ya mji wa Dodoma alipofanya ziara ya
kushitukiza, kukagua matumizi ya mashine za kutolea risiti kwa njia ya
kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara wa maduka mjii humo.
BENNY MWAIPAJA, DODOMA
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dokta
Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika mitaa ya mji wa
Dodoma na kubaini baadhi ya wafanyabiashara hawatumii ipasavyo mashine
za kieletroniki za kukusanyia kodi ya Serikali-EFDs na kuwaonya
wafanyabiashara kote nchini kuacha mchezo huo.
Dkt. Mpango aliyeambatana na
baadhi ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato hapa nchini-TRA mkoa wa Dodoma
amebaini baadhi ya wafanyabiashara hao wasio waaminifu hawatoi risiti
huku wengine wakiandika kiwango kidogo cha fedha kwenye risiti hizo.
Mmoja wa wafanyabiashara
aliyekumbana na mkono wa Waziri Dokta Mpango, ni Bwana ISDORI SHIRIMA
ambaye amekiri kufanya makosa ya kutotumia mashine hizi ipasavyo
“naomba unisamehe Mheshimiwa,
sitarudia tena unajua sisi vijana tunabangaiza, lakini nimebaini
nimefanya makosa” aliomba msamaha Bw. Shirima
Hata hivyo Dkt. Mpango ameiagiza
Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA mkoa wa Dodoma, kufanya ukaguzi wa kina
wa mahesabu ya mfanyabiashara huyo ili kubaini kiwango cha kodi
alichokwepa na kumchukulia hatua stahiki.
Aidha, Dokta Mpango ameiagiza
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Dodoma kuwapeleka ofisini kwake
mawakala wote mkoani humo wanaosambaza mashine za kieletroniki za
kukusanyia mapato EFDs baada ya kubaini kuwa zaidi ya mashine 100
zimeharibika na hazitumiki tangu jana.
“Kuna kitu sikielewi na hakiingii
akilini, inakuwaje mashine ziharibike kwa kiwango hicho, mashine 100
kuharibika kwa siku mbili ni nyingi na ina maana nimekosa mapato mengi”
alielezea kwa masikitiko Dkt. Mpango.
Aliagiza mawakala wote
wanaosambaza ama kuuza mashine hizo wakutane naye ofisini kwake mjini
humo ili kubaini tatizo na kuongeza kuwa haiwezekani wafanyabishara
walipie mashine hizo zaidi ya mwezi uliopita lakini hawapelekewi hali
inayozidi kuikosesha Serikali mapato yake.
Baadhi ya wananchi na
wafanyabiashara wamepongeza uamuzi wa Serikali wa kulivalia njuga suala
la kodi na kwamba wako tayari kuiunga mkono Serikali kwa kutoa risiti
wanapouza bidhaa na kudai risiti zenye viwango sahihi vya manunuzi
waliyoyafanya ili kuijengea Serikali uwezo wa kuihudumia jamii.
Dokta Mpango ametembelea pia
baadhi ya vituo vya mafuta mjini humo na kuwakumbusha wamiliki wote wa
vituo vya mafuta kuzingatia agizo la Serikali linalowataka wafunge
mashine maalumu za kielektroniki zinazofungwa kwenye pampu za mafuta
ndani ya siku 14 ambazo ziko ukingoni.










0 Comments