Uongozi wa
Klabu ya Singida United, imetoa basi lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 350
litakalotumiwa na wachezaji pamoja na benchi lao la ufundi katika msimu wa Ligi
Kuu Tanzania bara wa 2017/2018.
Kikosi a
Singida United kimerejea Ligi Kuu Bara Msimu huu na Leo Jumanne July 4, 2017 kitaingia
kambini mjini Mwanza chini ya Kocha wa zamani wa Yanga SC, Hans van der Pluijm
ndiye kocha anayekinoa kikosi hicho ambacho kinadhaminiwa na SportPesa.
Muonekano wa
gari la Singida United linaloratajiwa kutumiwa na wachezaji wa timu hiyo katika
msimu mpya wa Ligi kuu.
Katika basi
hiyo, Singida United imeweka picha za Rais wa timu hiyo, Mwingulu Nchemba
ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na picha ya mmiliki wa timu, Yusuf
Mwandami.
Meneja wa
klabu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati
wa kulitambulisha basi lao jipya litakalotumika kwa safari za ndani za timu ya
Singida United.
Basi hilo
aina ya Dragon lenye thamani ya Sh 350 milioni limezinduliwa rasmi na litaanza
kutumika katika safari za timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu 2017/2018.

0 Comments