
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akikabidhiwa fomu ya na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dodoma, Gama Juma, leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akikabidhiwa fomu ya na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dodoma, Gama Juma, leo.
Hayo
yametimia kufuatia Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Alhaji Bulembo kuchukua
fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo, katika Ofisi za Jumuiya
ya Wazazi mkoa wa Dodoma leo mchana, huku akifanya tukio hilo kimyakimya
tofauti na ilivyozoeleka ambapo baadhi ya wawania uongozi husindikizwa
na wapambe na waandishi wa habari.
Licha
ya kwenda kimyakimya, lakini taarifa zilizopatikana mjini hapa,
zimesema kwamba alifika kwenye Ofisi za hizo za Wazazi mkoa wa Dodoma
mda wa saa nane mchana akijiedesha kwa gari namba T888 DFB aina Toyota
Land Cruser lenye vioo vya giza, na kukabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti
wa Jumuia wa mkoa Gama Juma.
Mapema
mwaka huu Alhaj Bulembo alitamka katika katika moja ya vikao rasmi vya
Jumuiya ya Wazazi kwamba hatagombea tena nafasi yake ya Uenyekiti, kauli
ambayo ilidumu kwa mda mrefu lakini baadaye Baadhi ya Wazee akiwemo
Balozi Job Lusinde na baadhi ya viongozi na Wanachama wa Jumuia hiyo
wakanza kutoa kauli za kumsihi abatilishe uamuzi wake huo wa kutogombea
tena.
Maombi
hayo yaliripotiwa kutolewa kwa nyakati na sehemu tofauti hapa nchini,
wakiwemo Makatibu wa Jumuia hiyo kutoka mikoa ya Tanzania Bara na
Zanzibar, ambao kwenye Semina moja iliyofanyika mjini hapa, mwezi
uliopita, walimsihi Alhaj Bulembo kuchukua fomu huku wakisisitiza kwamba
ikibidhi watamlipia fedha za fumu hizo.
Kufuatia
mwaka huu wa 2017 kuwa mwaka wa Uchaguzi wa Viongozi ndani Chama Cha
Mapinduzi na Jumuiya zake ikiwemo Jumuiya hiyo ya Wazazu Tanzania na
Jumuia za Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), UVCCM kuanzia ngazi ya
Tawi hadi Taifa CCM ilitangaza kuanza kutolewa fomu kwa wanaohitaji
rudhaa za uongozi kwa ngazi hizo, kuanzia leo Julai 20217.
Kulingana
na msimamo wa sasa wa CCM baada ya mabadiliko makubwa iliyofanya
Dodoma, ambayo pamoja na kutaka kuwa na viongozi wenye nia za dhati na
wenye kuguswa na shida za wananchi, bila shaka wanaowania uongozi katika
kinyang'anyiro cha uchaguzi huo watalazimika kuwa wamejipima vya
kutosha kulingana na sifa zilizotajwa.
0 Comments