Random Posts

Hizi Hapa Faida Kula Bamia

Bamia ni mboga ambayo inafahamika na watu wengi na imekuwa ikitumiwa na watu wengi hapa nchini Tanzania.
Pamoja na bamia kuwa mboga, lakini pia ina faida nyingi katika miili yetu, licha ya kuwa wengi wetu huwa hatufahamu faida zake zaidi ya kula tu kama mboga.
Miongoni mwa faida za mboga hii ni pamoja na kusaidia kuondosha vimelea vya sumu kwenye ngozi, inasaidia pia kuimarisha afya ya nywele na kuongeza kinga ya mwili.

-Bamia husaidia kuondoa uchovu wa mwili na msongo wa mawazo pamoja na kusaidia kutibu tatizo la kukosa choo.
Aidha, bamia pia inaelezwa kusaidia kusafisha damu, kutibu mafua, vidonda vya tumbo, inaimarisha mifupa pamoja na kuwa kinga ya magonjwa kama utapiamlo na anemia.

Ni msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo ya mifupa au maumivu ya viungo kwani huongeza uteute kwenye viungo vya mifupa, ili upate faida hii inakupasa ule bamia kama supu/mchemsho
Mbali na hayo bamia pia inasaidia kutibu  magonjwa  mbalimbali  ya  zinaa  kama vile  kaswende na kisonono. Vilevile  inaponya  tatizo  la  kwenda  hedhi  mara  kwa  mara na  chango la kike.

Hizo ni baadhi ya faida za ulaji wa bamia

Post a Comment

0 Comments