Wakati Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikiwa imetoa ongezeko la siku 15 kwa wadaiwa wa
Kodi ya Pango la Ardhi kuendelea kufanya malipo hayo; Vituo mbalimbali vya Makusanyo
hayo vimeonekana kufurika.
Katika
picha ni Maeneo kadhaa tu nchini, ambapo Wananchi wameendelea kujitokeza
kufanya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi.
Kituo cha Makusanyo- Kivukoni, Magogoni (Dar es Salaam)
Hatahivyo, Malipo ya Kodi ya
Pango la Ardhi yameboreshwa hivi karibuni kwa Mfumo Mpya wa Kielektroniki
ambapo mdaiwa ana uwezo wa kufanya malipo hayo kwa njia ya simu ya Mkononi au
kwa kuingia; (http://landrent.lands.go.tz/landrent).
Aidha, tathimini imeonyesha
kuwa baadhi ya Wananchi wameshafanikiwa kufanya malipo haya kwa kutumia Mfumo
huu Mpya wa Kielektroniki.
Na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.





0 Comments