Mbali ya hilo,Issango anadaiwa kushindwa kusimamia mkakati wa serikali wa kudhibiti makosa ya usalama barabarani yanayosababisha ajali.
Aidha ametoa maelekezo kwa kamanda wa polisi mkoani Pwani,kuhakikisha mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mwingine atakaepangwa mkoani hapo afanyekazi ipasavyo na kama kuna changamoto wazieleze ili ziweze kuangaliwa namna ya kuzitatua.
Katika hatua nyingine ,Masauni ametoa siku tatu kwa askari wa usalama barabarani kuhakikisha wanawakamata madereva wa bodaboda ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani.
Masauni alitoa msimamo huo,kwenye stendi ya Mailmoja ya mabasi yaendayo mikoani ,wakati wa ziara yake ya kutembelea utendaji kazi wa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani humo.
Alisema wameanza kula sahani moja na watendaji wazembe ,wasiokwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
Masauni aliwataka makamanda wengine wa usalama barabarani wilaya na mikoa ambao hawawajibiki wajiandae.
Alieleza askari ama mtumishi yeyote aliechini ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi ajitume kikamilifu kwani serikali hii haitowavumilia wale wasioweza kutimiza majukumu yao.
“Rto huyo amekaliwa vibaya hawezi kusimamia maelekezo anayopewa,hivyo kazi imemshinda achukuliwe hatua za kinidhamu ,serikali haiwezi kuwavumilia askari ambao hawatekelezi majukumu na maelekezo wanayopewa kwa maslahi ya wananchi”
“Hatuwezi kuona wananchi wanaendelea kufa na kujeruhiwa kwenye ajali,mkakati wa serikali ni kupunguza na kuondoa ajali zembe kwa kuzidhibiti,badala ya kuongezeka”alisema Masauni.
Alieleza waliwahi kufanya ukaguzi wa mabasi na vituo vya mabasi katika kipindi cha nyuma na kugundua mapungufu ya utekelezaji wa ukaguzi hasa kwa askari wa usalama barabarani ikiwemo Kibaha -barabara kuu ya Morogoro
Masauni alisema kati ya mapungufu hayo ni sanjali na idadi ndogo ya askari na nyenzo wakatoa maelekezo kwa RTO huyo ,ahakikishe anarekebisha mapungufu hayo lakini cha kusikitisha hakuna kilichotekelezwa hadi sasa.
“Wapo madereva wa mabasi wanashirikiana na askari hao wasio na uadilifu baadhi ya mabasi kutoka mikoani hayakamatwi licha ya kuendesha kwa mwendo kasi ili kuwahi kufika Dar es salaam.
“Na yapo mabasi yanatekeleza sheria za usalama barabarani kwa kuendesha kwa kufuata sheria na yanafika saa mbili ama saa tatu huku mengine yakifika saa 11 bila kukamatwa wakati yanatoka eneo moja”alisisitiza Masauni.
Hata hivyo alibainisha ,aliwahi kutoka Maili Moja alipofika Chalinze alibadilisha namba za gari lake za Uwaziri na kuweka namba za STK na kumwamuru dereva wake aendeshe gari kwa mwendo wa kasi hadi Bagamoyo na hakuna askari wa usalama aliyesimamisha gari hilo.
“Pia natoa siku tatu kwani hapa naona madereva wa bodaboda wanavunja sheria mbele ya macho yetu wanabeba mishikaki ,hawajavaa kofia ngumu na pale Chalinze tuliwaona hawana kofia hata moja hili haliwezi kukubalika’alisema Masauni.
Masauni alieleza,haiwezekani naibu waziri ,kamanda wa usalama barabarani nchini, wanaacha shughuli za kitaifa na kwenda kusimamia eneo mojamwakati watendaji wapo.
Nae kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini,kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi, Fortunatus Musilimu ,alisema kumekuwa na matatizo ya usimamizi na kiutendeji kwa baadhi ya askari wa usalama barabarani.
Kwa mujibu wa Musilimu, watahakikisha wanasimamia kikamilifu sheria za usalama barabarani ili kuwadhibiti madereva ambao wanakiuka sheria kwa kuwachukulia hatua kali.
0 Comments