MBUNGE wa Dodoma mjini, Anthony
Mavunde leo ameshirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nzasa,Kata ya Chihanga
katika ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na matundu ya vyoo.
Ujenzi huo unahusisha nyumba tatu za
walimu, ,madarasa matatu na matundu ya vyoo 7.
Katika ujenzi huo, unatarajiwa
kugharimu Sh.205,500,000 ambazo zinazotokana na mradi wa ‘Pay 4 Results’(P4R)
uliopo chini ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
Akizungumza na wananchi hao, Mavunde ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, aliwapongeza kwa kujitolea
kuhakikisha mradi unafanikiwa.
Alibainisha kuwa changamoto
zilizokuwa zikiikabili shule hiyo ni kukosekana kwa nyumba za walimu na hivyo
kuwafanya walimu kuishi umbali wa kilomita zaidi ya 25.
Mbali na hilo alisema kulikuwa na
upungufu wa madarasa pamoja na uchakavu wa vyoo.
Wananchi wa Nzasa wakishiriki
katika ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi ya Nzasa wakiwa na Mbunge wao
Anthony Mavunde.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akimsikiliza mmoja wa wazee wa kijiji cha Nzasa.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akishiriki ujenzi wa moja ya majengo ya shule ya msingi Nzasa akiwa na
wananchi wake.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akishiriki ujenzi wa moja ya majengo ya shule ya msingi Nzasa akiwa na
wananchi wake.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Nzasa
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Nzasa
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nzasa katika ujenzi wa majengo ya
shule ya msingi.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akimsikiliza mmoja wa viongozi wa kijiji hicho.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule
ya msingi Nzasa.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akibeba zege kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya
msingi Nzasa.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony
Mavunde akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule
ya msingi Nzasa.











0 Comments