Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Segerea
alipofanya ziara ya kikazi ili kupokea
maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Tawala wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Edward Mpogolo akiwatambulisha
baadhi ya watumishi na viongozi wa Segerea waliohudhuria kikao kazi kilichowakutanisha
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) Jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Jimbo la Segerea, Mhe. Bonnah Kaluwa akitoa salamu wakati wa kikao kazi na
kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), leo Jijini Dar es Salaam.
Meneja
Masoko kutoka kampuni ya Watumishi (Watumishi
Housing Company), Bw. Raphael Mwabuponde, akiwasilisha mada kuhusu taratibu
za kupata nyumba kwa Watumishi wa Umma wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah
J. Kairuki (Mb) na Watumishi wa Umma wa Segerea, Jijini Dar es Salaam.
Mtumishi
wa Umma kutoka Tabora, Bw. John Joseph akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi
kilichowakutanisha watumishi wa umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kutoka
Segerea na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkazi
wa Segerea, Bw. Juma Kali akiwasilisha hoja maalum wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala - Segerea na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar
es Salaam.
................................
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) amezitaka Taasisi za Serikali kuratibu suala la
uhamisho wa watumishi wa umma kwa makini pale inapohitajika kufanya hivyo Ili
kuepuka kero na usumbufu kwa watumishi.
Waziri
Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala eneo la Segerea, jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Kairuki amesema uhamisho lazima ufanyike kwa mtumishi wa umma endapo kukiwa na
sababu za msingi sana. “Naomba ieleweke kuwa uhamisho una taratibu zake hivyo
kila mwajiri ni mwajiri akazifuata.” Mhe. Kairuki alisisitiza.
Ameongeza
kuwa imebainika wapo baadhi ya watumishi wa umma wanawasilisha sababu
mbalimbali kwa waajiri kuomba kuhama wakiwa na nia ya kukwepa kukaguliwa sifa
zao za elimu.
Waziri
Kairuki amesisitiza kuwa uhamisho usifanyike kwa mtumishi ambaye anaonekana
kuwa na matatizo.
“Baadhi
ya waajiri wamekuwa na tabia ya kuwahamisha watumishi wa umma ambao wameonekana
kuwa na tatizo na kuwahamishia sehemu nyingine, uhamisho wa namna hii
haukubaliki, tatizo la mtumishi linatakiwa kufanyiwa kazi kwenye kituo chake
cha kazi na sio kupeleka tatizo sehemu nyingine.” Mhe. Kairuki ameongeza.
Mhe.
Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama ambapo leo ni
siku ya tisa akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala-Segerea kwa kukutana
na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.
Waziri
Kairuki katika vikao kazi amehimiza watumishi wa umma nchini kubadili mtindo wa
maisha, kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi, kujiepusha na ugonjwa wa UKIMWI,
na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa (MSY).
Lengo
la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na
changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi
na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo
yaliyopangwa na Serikali.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI
YA RAIS-UTUMISHI
20.07.2017
0 Comments