Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya
Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) katika
kikao cha siku moja ukumbi wa Ikulu Mjini
Unguja
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati
Zanzibar(ZURA) Ng,Haji Kali alipokuwa akitoa mchango na kuelezea
maendeleo waliofikia katika Mamlaka hiyo walipokuwa na Kikao cha siku
moja cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira na Uongozi
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na
Nishati Zanzibar (ZURA) ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa Mwenyekiti wa
Kikao hicho kilichofanyuika Ikulu Mjini Unguja,
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Huduma ya Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) wakiwa katika mazungumzo na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu MJini Unguja.
[Picha na
Ikulu.]



0 Comments