Awataka
Wawekezaji Kutumia Fursa Zilizopo Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli (katikati) akifuatilia sherehe za uzinduzi wa Maonesho ya
41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) leo Jijini Dar es Salaam.
Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba)
vilivyoko barabara ya Kilwa, kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Ukuzaji wa
Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Afri Tea Bw.
Abdulkarim Mulla tuzo ya jumla ya wasambazaji bora wa bidhaa za ndani za
vyakula nchini wakati wa sherehe za uzinduzi wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya
Kimataifa Dar es Salaam (DITF) leo Jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo
yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba) vilivyoko
barabara ya Kilwa, kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Ukuzaji wa Biashara kwa
maendeleo ya Viwanda”.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya bidhaa za ngozi za zilizotengenezwa
hapa nchini alizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Biashara
Tanzania (TANTRADE) Mhandisi. Christopher Chiza mara baada ya kuzindua rasmi
Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) leo Jijini Dar es
Salaam. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere
(Sabasaba) vilivyoko barabara ya Kilwa, kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Ukuzaji
wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”.
Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Biashara ya
Kimataifa Dar es Salaama maarufu kama sabasaba wakifuatilia hafla ya uzinduzi
rasmi wa maonesho hayo leo Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maonesho hayo
mwaka huu ni “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akichukua nembo yenye alama za bendera za mataifa ya
Tanzania na Ujerumani alipotembelea banda la linalotumiwa na wafanyabiashara
kutoka Ujerumani leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Balozi wa Ujerumani
nchini John Reyels.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE, Mhandisi Christopher Chiza wakipunga mkono
wakati wakimuaga Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi katika
hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam
(DITF) leo. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere
(Sabasaba) vilivyoko barabara ya Kilwa, ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo
mwaka huu ni “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda”.
...............
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Mabalozi na Wawekezaji
wa ndani na nje ya nchi kutumia fursa za uwekezaji zilizopo nchini na kuisaidia
miradi mikubwa ya kiuchumi ili iweze kuleta tija na maendeleo ya haraka kwa
Watanzania.
Akifungua maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam leo,
Rais Magufuli alisema Serikali ya Awamu ya tano itaendelea na dhamira yake ya kuhamasisha
na kuimarisha mazingira ya uwekezaji ili kuhakikisha kuwa Watanzania
wananufaika na rasilimali zilizopo ndani ya nchi yao.
Rais Magufuli alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea
kushughulikia kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakwaza wawekezaji ikiwemo utitiri
wa kodi, ambapo katika bajeti ya mwaka 2017/18 Serikali imeondoa na kufuta kodi
mbalimbali ili kuhakikisha kuwa dhamira ya ujenzi wa uchumi wa viwanda
inafikiwa.
Aidha Rais Magufuli alisema katika kutimiza malengo ya uchumi wa
Viwanda, Serikali imekusudia kufufua mradi wa kuzalisha umeme
kwa kutumia nguvu za maji wa Stiegler’s Gorge wenye uwezo kuzalisha kiasi cha
megawati 2100 za umeme, sambamba na kuongeza kiasi cha megawati 600 katika
mradi wa kinyerezi III.
“Unapozungumzia
Viwanda ni lazima uwe na umeme wa uhakika, hivyo Serikali ya Awamu ya Tano imechukua
hatua muhimu kwa kufufua mradi wa Stiegler’s
Gorge kwa kutumia fedha zetu za ndani, kupitia mradi huu tutakuwa tumepata eneo
la maji na kuhifadhi mazingira” alisema
Rais Magufuli.
Aliongeza malengo
ya Serikali ni kuwa na idadi kubwa zaidi ya viwanda vitakavyowezesha Watanzania
kupata ajira, hivyo aliwataka Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nje kutumia
maonesho hayo kwa ajili ya kubaini fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo
nchini.
Rais Magufuli pia
aliwataka Wafanyabiashara hao kutumia fursa za maonesho hayo kwa ajili ya
kubadilishana uzoefu katika maeneo ya teknolojia na kuimarisha ubia wa
kibiashara miongoni mwao, na pia kutumia fursa ya kukutana na wateja kwa ajili
ya kubaini mahitaji na mapungufu ya bidhaa zao.
Kwa upande wake
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Wizara zimepanga
kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kuhamasisha Wawekezaji wanajitokeza katika
ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.
“Katika maonesho
haya kuna taasisi muhimu zinazohusika moja kwa moja katika suala zima la
uwekezaji, TBS, SIDO, BRELA, TRA wapo katika maonesho haya kwa ajili ya masomo
yanayohusu miongozo yote kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini” alisema
Mwijage.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Mhandisi Christopher Chiza katika
kuunga mkono na kuhamasisha kwa vitendo dhamira ya kufikia uchumi wa kati
kupitia Viwanda ambapo kuanzia mwaka jana TanTrade imekuwa ikifanya maonesho ya
viwanda kwa wajasiriamali mbalimbali.
Aliongeza kuwa malengo ya maonesho hayo ni kutoa fursa kwa
Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuweza kutumia fursa ya rasilimali
mbalimbali zilizopo nchini zinaweza kutumia katika kuinua uchumi wa Watanzania.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa Bodi alitangaza
kuongeza siku tano za maonesho ambapo sasa maonesho hayo yanatarajiwa
kumalizika Julai 13 bada ya Julai 8 kama ilivyotangazwa awali.






0 Comments