Klabu ya Singida United imetambulisha ramsi basi lake jipya itakalotumia kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Basi hilo lenye thamani ya Sh 350 milioni limezinduliwa rasmi
na litaanza kutumika katika safari za timu hiyo iliyopanda daraja msimu
huu.
Katika basi hiyo, Singida imeweka picha za Rais wa timu hiyo,
Mwingulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na picha ya
mmiliki wa timu, Yusuf Mwandami.
Ofisa Habari wa timu hiyo, Festo
Sanga alisema wataanza maandalizi yao hivi karibuni ili kujiandaa na
msimu mpya wa Ligi Kuu huku wakitarajia kukamilisha usajili wa nyota
wachache waliosalia.

0 Comments