Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa kada
mbalimbali wa Tarafa ya Ukonga alipofanya ziara ya kikazi ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero
za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) akifafanua hoja mbalimbali alizopokea kutoka kwa
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala – Tarafa ya Ukonga (hawapo
pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao leo Jijini Dar es Salaam. Kulia
kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Msongela Palela na
kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Edward
Mpogolo.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Furaha, Bw. Daniel
Song’oa akiwasilisha malalamiko yake wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala – Tarafa ya Ukonga na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar
es Salaam.
Sehemu
ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala – Tarafa ya Ukonga
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa kikao
kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
...........................
MISHAHARA KUPITIA
FOMU
Ofisi
ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuanzia tarehe 31
Oktoba, 2017 imeelekeza madai ya malimbikizo ya mishahara ya Watumishi wa Umma
kwa kujaza fomu za madai kufikia ukomo. Maafisa Utumishi wanatakiwa kupokea na kujaza
madai hayo kupitia Mfumo wa Taarifa Shirikishi za Kiutumishi na Mishahara.
Waziri
Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Tarafa ya Ukonga, kilichofanyika ukumbi wa
mikutano wa shule ya Sekondari ya Pugu, jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Kairuki amesema katika kikao kilichowakutanisha watumishi wa umma kutoka kata
13 za Ukonga kuwa kumekuwa na adha kubwa ya mlundikano wa makaratasi ambao
umekua ukichelewesha watumishi wa umma kupata haki zao kwa wakati kwa kupitia
hatua mbalimbali, hivyo kuanzia tarehe 31 Oktoba, 2017 kila hatua itafanyika kielektroniki
ili kuleta mabadiliko na kuboresha utendaji kazi.
“Nawaagiza
waajiri kupitia kwa Maafisa Utumishi kuingiza taarifa za malimbikizo ya
mishahara ya watumishi wa umma kwa usahihi ili mfumo uweze kukokotoa moja kwa
moja na malipo kufanyika haraka” Mhe. Kairuki amesema.
Ameongeza
kuwa Maafisa Utumishi wawe makini katika kupokea na kujaza taarifa za watumishi
wa umma katika mfumo, pia watumishi nao watoe ushirikiano wa dhati katika
kuweka kumbukumbu za taarifa zao ili wapate haki yao inavyostahili.
Aidha,
Waziri Kairuki amesema Serikali inaendelea kupitia muundo wake upya ili kupunguza
ukubwa, kuunganisha taasisi zinazofanya kazi zinazofanana na kuleta uwiano sawa
wa stahili kwa watumishi wa umma serikalini.
“Huko
nyuma, tumeshuhudia baadhi ya taasisi za Serikali zikijipangia stahili mbalimbali
pamoja na mishahara, sasa hivi ni lazima kuomba kibali kwa Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora” Mhe. Kairuki amesema
na kusisitiza lengo ni kuwa na uwiano sawa.
Ameongeza
kuwa Serikali ina nia nzuri na inaijali rasimaliwatu yake ambapo katika zoezi
hili tathmini ya kazi inafanyika ili kila kada itendewe haki katika kupata
stahili kulingana na majukumu yake.
Waziri
Kairuki katika ziara yake amewataka watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano na
kuwasisitiza Maafisa Utumishi kuwasikiliza wateja wao, wakiwamo watumishi
wenzao na kuwapatia huduma stahiki ikiwa ni pamoja na kuwaelemisha kuhusu nyaraka
za kiutumishi.
Awali
akisoma taarifa ya Tarafa ya Ukonga, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala, Bw. Msongela Palela amempongeza Mhe, Kairuki kwa kufanya ziara hizo
kwani imewasaidia watumishi wa umma kujua masuala mengi ya kiutumishi.
“Mimi
nina mwaka mmoja tangu niingie Halmashauri ya Manipaa ya Ilala lakini kwa ziara
hizi nimejifunza masuala mengi sana ya kiutumishi na hata kwa watumishi
wenzangu nina hakika malalamiko mengi yatapungua,” Bw. Palela
Mhe.
Kairuki anahitimisha ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama ambapo leo
amekutana na Watumishi wa Umma wa kada zote wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,
Tarafa ya Ukonga.
Vikao
kazi vilivyofanyika mkoani Dar es salaam, pamoja na ufafanuzi uliotolewa, zaidi
ya hoja 750 zimepokelewa kwa njia ya maandishi ili kufanyiwa kazi.
Lengo
la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto
zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta
mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo yaliyopangwa na
Serikali.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI
YA RAIS-UTUMISHI
21.07.2017




0 Comments