Mjumbe wa kamati ya
kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Mussa Mbaruku akizungumza
jambo pale kamati hiyo ilipokutana na viongozi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa lengo la kuwapitisha Wajumbe wa kamati
kuhusu hesabu za fedha za Taasisi husika, katika kikao kilichofanyika leo Mjini
Dodoma. kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Juma Aweso
Mjumbe wa kamati ya
kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga akiongoza kikao
cha kamati hiyo pale ilipokutana na
viongozi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa
lengo la kuwapitisha Wajumbe wa kamati kuhusu hesabu za fedha za Taasisi
husika, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
Wajumbe
wa kamati ya
kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakifuatilia mazungumzo
baina yao na Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi lengo likiwa ni
kupitia Mahesabu na Maagizo ya kamati hiyo, katika kikao kilichofanyika
leo Mjini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.
Naghenjwa kaboyoka(katikati).
Mwenyekiti wa Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Vedasto Ngombale
(katikati) akiongoza kikao cha kamati hiyo dhidi ya viongozi kutoka Ofisi ya
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Hazina na Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika kikao kilichofanyika leo Mjini
Dodoma.kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Abdallah Chikota na
kulia ni katibu kamati wa Bunge, Ndg. Dismiss Muyanja
(PICHA
NA OFISI YA BUNGE)




0 Comments