Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi
Sihaba Nkinga akizungumza na Maafisa
Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa wakati alipofanya
ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub akisistiza jambo kwa kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa
Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi
Sihaba Nkinga alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya
Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick
Golwike akifafanua jambo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii
Mkoani Iringa wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipofanya
ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na
Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati Katibu Mkuu huyo
alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya
Jamii.
Kikundi cha Sanaa cha Malezi na Uhamasishaji
wa Ulinzi kwa Mtoto Wilaya ya Iringa wakiimba wimbo wa kumshukuru Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga kwa kuendelea kuhamasisha Maafisa
Maendeleo ya Jamii na ustawi wa JAmii kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi
Sihaba Nkinga(kulia) akijadiliana jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi
Waumoja Ayoub mara baada ya kumalizika
kwa kikao kati ya Katibu Mkuu huyo na Maafisa Maendeleo ya jamii na Maafisa
Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa.
Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
.....................................
Na
Raymond Mushumbusi WAMJW
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto anayeshughulikia
Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amewaasa maafisa Maendeleo
ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii nchini kuamsha ari ya kufanya kazi kwa
wananchi ili kujiletea maendeleo.
Ameyasema
hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa
Ustawi wa Jamii mkoani Iringa alipokuwa akifanya ziara kujionea utekelezaji wa
Sera ya Maendeleo ya jamii nchini.
Bibi
Sihaba Nkinga ameongeza kuwa viongozi wa Halmashauri na Mikoa nchini wanatakiwa
kuwapa nafasi Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili
kurejesha ari ya wananchi kujitolea katika kutekeleza shhughuli za kimaendeleo
katika maeneo yao.
“
Nawaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii mtimize majukumu
yenu ipasavyo ili kuamsha ari ya ufanyaji kazi kwa wananchi ili kuleta
maendeleo katika maeneo yao” alisema Bibi Sihaba.
Katibu
Mkuu Bibi Sihaba Nkinga pia amesisitiza matumizi ya rasilimali zilizopo ili
kuendelea kuhimiza wananchi kujitolea katika kujitolea na kufanya kazi
zitakazowaletea maendeleo katika maeneo yao.
Aidha
kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub amemuakikishia Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga kuwapa ushirikiano Maafisa Maendeleo ya
Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili waweze kutimkiza majukumu yao.
“Sisi
viongozi wa mkoa tupo tayari kutoa ushirikiano kwa Maafisa hawa ili kuwawezesha
kutimiza majukumu yao kwa wakati na katika ufanisi” alisema Bibi Waumoja.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia
Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amefanya ziara mkoani Iringa
kwa lengo la kujionea utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii na kuamsha
aerinya wananchi katika kujitolea kufanya kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.








0 Comments