Mmoja
wa wananchi kutoka Wilaya ya Temeke (aliyesimama) akieleza kero yake kwa Mhe. Lukuvi
wakati wa kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi.
Mhe.
William Lukuvi akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika ofisini kwake kwa ajili
ya kutoa kero zao za masuala ya ardhi.
............................
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mhe. William Lukuvi, amekutana na wakazi wa Wilaya ya Temeke na
Kigamboni katika kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi.
Katika mahojiano
na wananchi hao, Mhe. Lukuvi amewaonya wananchi kuwa makini na matapeli
wanaochukua nyaraka halali za umiliki na kutengeza nyaraka feki.
Hayo yamebainika baada ya baadhi ya
wananchi kulalamikia mmliki wa kampuni ya Holland
Investment iliyopo jijini Dar es
Salaam kwamba, amekuwa akichukua nyaraka halali za umiliki kwa wananchi kwa
lengo la kuwasaidia na baadae kuwabadilishia na kuwarudishia nyaraka feki.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
0 Comments