Mwezeshaji kutoka Mradi
wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) Christopher Masaaka ambaye pia ni Afisa
Uchumi kutoka Halmashauri ya Wangingómbe
Mkoa wa Njombe akitoa mafunzo kwa moja ya kundi la washiriki wa mafunzo ya
Mfumo wa Kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na
Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Wagisha Ronald
na Hussein Kiranga (Katikati) kutoka Taasisi ya GIZ-TGPSH.
Baadhi ya Maafisa
Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Manispaa ya Singida wakijadili jambo
wakati wa mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa
Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi
mbalimbali wakiwemo Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Halmashauri
za Mkoa wa Manyara wakifuatilia mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep)
iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za
Mitaa yanayoratibiwa na Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) kwa
kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) leo Mjini
Dodoma.
(Picha
na Beatrice Lyimo-MAELEZO)



0 Comments