Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg. John L.Kayombo kwa
kushirikiana na Madiwani wakiongozwa na Mstahiki Meya Boniface Jacob,,pamoja na
maofisa wa TANROADS,Mkandarasi wa mradi wa Interchange-CCI-CCE,Jeshi la
polisi,wenyeviti wa mtaa na watendaji wa kata za Makuburi,Sinza na Ubungo wamekutana na wanyabiashara maarufu kwa jina
la Machinga na mama lishe ambao wanafanya biashara zao pembezoni mwa
barabara ya Morogoro Road
makutano na Mandela road Ubungo
mataa sehemu ambayo Mradi wa barabara za
juu (Interchange) unatarajia kuanza kujengwa.
Lengo la Mkutano huo lilikuwa ni kuongea na wafanya biashara
hao kuwataka kuondoka katika eneo hilo
ili kupisha ujenzi wa Barabara hizo za juu zinazotarajiwa kuanza kujengwa hivi
karibuni ambazo zitarahisha usafiri na kuondoa kero za foleni ambazo zimedumu
kwa muda mrefu.
Uongozi huo umeelekeza wamachinga hao na mama lishe eneo la kwenda ambapo umewaahidi kuwapeleka
katika eneo la mawasliano Simu 2000 na
kupatiwa sehemu za kufanya biashara zao katika soko hilo kwa utaratibu
maalum.Na wale watakaoona wanaweza kwenda sehemu nyingine ambayo si eneo la
mradi wamepewa fursa hiyo pia.
Akiongea katika mkutano huo Mstahiki Meya wa Mnispaa ya Ubungo amewasihi wamachinga
hao kuondoka wenyewe pasipo kutumia
nguvu yani kwa amani bila kutumika kwa nguvu ya jeshi la polisi kwa kuwa mradi
huo ukitekelezwa unawanufaisha wananchi
wote wa Ubungo na Taifa kwa Ujumla.
Nae Mkurugenzi akisisitiza katika hilo amesema ili
mkandarasi aendelee na kazi anahitaji eneo husika kuwa wazi ili waweze kufanya
kazi kwa ufanisi., alisema ninyi ni moja ya wananchi watakaonufaika na mradi
huu hivyo kwa pamoja tunatakiwa kutoa ushirikiano ili kumrahisishia Mkandarasi
aweze kuanza kazi hii ya ujenzi mara moja kwa kuacha eneo la mradi
wazi,utaratibu umewekwa wa jinsi ya kupata eneo mtakalohamia ili muendelee
kufanya biashara SIM2000.
Pamoja na kupewa maelezo hayo wamachinga walipata nafasi ya
kuonyeshwa mipaka ya eneo la mradi ambalo linatakiwa liwe wazi kwa ajili ya
ujenzi kwa kuenyeshwa alama zilizowekwa.Pia walipata nafasi ya kujibiwa maswali
yao mbalimbali katika mkutano huo.
Wamachinga hao walipewa nafasi ya kuchagua wapewe siku ngapi
za kujipanga kuhama eneo hilo ambapo wamesema siku tatu kuanzia leo zitawatosha
kujipanga kuhama,pamoja na hilo mama lishe wa eneo hilo wamepewa nafasi ya
kuendelea kuwapikia mafundi watakaokuwa wanajenga au kufanya vibarua katika
ujenzi huo kwa utaratibu maalum watakaopewa pia na wengine watakaotaka kupata
nafasi ya vibarua katika ujenzi fursa hiyo pia wataipata kwa kufuata utaratibu.
Utekelezaji wa Mradi wa Barabara za Juu katika eneo la
Ubungo Mataa ni Muendelezo wa Miradi ya Barabara za Juu (Interchange) katika jiji la Dar es Salaam ambayo serikali
ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais John
Pombe Magufuli amedhamiria kuitekeleza ili kurahisisha usafiri na kisha
kurahisisha shughuli za uchumi kwa ujumla.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA
UHUSIANO UMC



0 Comments