Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na watumishi wa hospitali inayomilikiwa na Kanisa ya inayoitwa Dkt.Artiman iliyopo manispaa ya sumbawanga,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt.Khalfan Haule na kuliani ni Afisa Tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali
Msimamizi wa hospitali hiyo sister Yasinta Rugabo akisoma taarifa ya hospitali hiyo
Na.WAMJW-Rukwa
Viongozi wa Mkoa wa Rukwa wametakiwa kusimamia fedha za dawa
pamoja na upatikanaji wa dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya
vilivyopo kwenye mkoa huo
Waziri wa Afya,naendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na watoto
Ummy Mwalimu ameyasema hayo jana wakati akiongea na viongozi na watumishi wa
Wilaya na mkoa wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani hapa
Nahitaji mfamasia awe anaprinti karatasi yenye kuonyesha
dawa zilizopo kwenye stoo yake ili mganga anayeingia zamu siku hiyo aweze kujua
dawa zilizopo na kumuandikiamgonjwa wake kuliko kuanmdika dawa ambazo hazipo
kituoni hapo
Aidha Waziri Ummy aliwapongeza mkoa huo kutokana na kuwa na
hali nzuri nya uwepo wa dawa katika vituo vyote alivyotembelea ingawaje bado
kuna changamoto ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu uchangiaji wa dawa na
kuwataka wakimaliza dawa walizonazo stoo zikiisha wanatakiwa kupunguza bei za
dawa ili wananchi waweze kupata dawa hizo pasina shaka
Mheshimiwa Rais alisema hataki kuona wananchi wanapata shida
ya upatikana wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali hivyo
akaongeza bajeti ya dawa kwa miaka miwili mfululizao?akitolea mfano kwa mkoa wa
Rukwa ,mwaka 2016/2017 bajeti ya dawa iliongezeka kutoka milioni 495 hadi
kufikia bilioni 1.4 na kwa mwaka huu 2017/2018 imeongezwa na kufikia bilioni
2.02.
Hata hivyo alisema upatikanaji wa dawa huo utaongezeka
kutokana na kwamba hivi sasa serikali kupitia bohari ya dawa(MSD) inanunua dawa
moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wa ndani tofauti na zamani ambapo walikua
wakinunua toka kwa mawakala
Waziri Ummy aliwapongeza Mkoa huo licha ya changamoto zote
zinazowakabili katika vituo vya kutolea huduma bado mkoa huo unasonga mbele
katika kukabiliana na tatizo la vifo vitokanavyo na na uzazi kwa vifo 117 kati
ya vizazi hai laki moja wakati takwimu za kitaifa ni vifo 506
Kwa upande wa vifo vya watoto chini ya miaka mitano
wamepunguza na kuwa na vifo 31 kati ya
vizazi hai laki moja ambapo takwimu za kitaifa ni 67,aidha kwa akina mama
wajawazito wanaoenda kujifungulia kwenye vituo vya afya mkoa wa Rukwa ni akina
mama 65 kati ya mia moja ambapo takwimu za kitaifa ni akina mama 64,?hapa
niwapongeze mmepiga hatua sana?
Kutokana na jitihada za serikali za kupunguza vifo vya akina
mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano hivi karibuni ilinunua na
kusambaza kwenye halmashauri zote vitanda ishirini na tano ikiwemo vitanda
vitano kwa ajili ya kujifungulia pamoja na mshuka hamsini
Awali Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe.Justine Haule aliishukuru Serikali kwa kuwapatia vitanda
pamoja na mashuka na hivyo kupunguza changamoto ya vitanda katika wodi za akina
mama wanaojifungua na alitaka changamoto kubwa ni kwamba mji wa rukwa
unaendelea kukua hivyo bado huduma za afya zinahitajika sana ili kuweza kutoa
huduma bora kwa wananchi



0 Comments