Na Jonas Kamaleki – MAELEZO
Serikali kushirikiana na sekta
binafsi wanaweza kujenga msingi wa kitaifa katika kuimarisha
Usalama katika ulimwengu mzima kwa ujumla na kudondokana na
uhalifu wa kimitandao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam
na Naibu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Matt
Sutherland wakati wa ufunguzi wa Warsha ya masuala muhimu
katika kuweka miondombinu ya kiusalama katika mitandao.
Sutherland amesema kuwa uhalifu wa
kimitandao haungalii mipaka ya nchi bali unaweza kutokea
mahali popote na wakati wowote. Alisisitiza hilo amesema
kuwa mwezi Mei mwaka huu shambulio la kimtandao lilipiga
mifumo karibu nchi 100 Duniani..
“Katika shambulio hilo, Uingereza
tuliathirika sana hasa katika sekta ya Afya ambapo kompyuta
katika Hospitali nyingi zilishindwa kufanya kazi na
kusababisha madaktari kushindwa kupata taarifa za wagonjwa,
” alisema Sutherland .
Ameongeza kuwa Septemba mwaka jana
wakati lilipotokea tetemeko la ardhi Mkoani Kagera,
Uingereza ilikuwa mstari wa mbele katika kurejesha
miondombinu ya shule ya sekondari Ihungo kwani katika tukio
hilo waliotharika zaidi ni wanafunzi.
Akiongelea suala la kiusalama, Naibu
Balozi huyo amesema kuwa katika Mkutano wa Kilele
utakaofanyika mwakani utangalia masuala mbalimbali ya
kiusalama ikiwemo kupambana na ugaidi wa kimataifa,uhalifu
wa makusudi, mashambulio ya kimtandao utumwa mambo leo
na vitisho vya demokrasia.
Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Warsha,
Dkt. Martin Koyabe kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya
ya Madola (CTO) amesema kuwa lento la Warsha hii ni
kuwawezesha watumishi wa umma na wa sekta binafsi kufahamu
miondombinu ya kiusalama katika sekta muhimu za kiuchumi ili
kuleta maendeleo nchini.
Aidha, Dkt Koyabe amesema kuwa warsha
hii inakusanya watumishi pamoja ili kuwa uelewa wa kuainisha
maeneo muhimu ya kiuchumi yanayotakiwa mifumo yake ya
kimitandao kulindwa ili uchumi usiathirike endapo mifumo
hiyo inashambuliwa.
“Serikali ni muhimu kutunga sera,
sheria na kanuni za kuweka ulinzi wa kimitandao ili
tusiathirike wakati shambulio linapotokea,” alisema Dkt.
Koyabe
Ameongeza kuwa zipo changamoto kadhaa
katika kutekeleza programu za ulinzi wa kimitandao.
Amezitaja changamoto hizo kuwa ni ufinyu wa bajeti, uhaba wa
wataalaam na utaalaam katika eneo la ulinzi wa kimitandao.
Warsha hii ni mwendelezo wa juhudi za
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na CTO katika
kukamilisha Mkakati wa Kitaifa wa Usalama wa Kimitandao
(National Cyber Security Strategy).

0 Comments