
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akifafanua mapato na matumzi ya Taasisi hiyo katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Gimbi akizungumza kuhusu umuhimu wa kuwashirikisha watumishi katika uandaaji wa bajeti katika mkutano wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Tulizo Shemu.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akielezea umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichopfanyika leo jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha na JKCI
Na Mwandishi Maalum
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma, kuongeza ufanisi na kutoa huduma bora kwa wagonjwa ili epukana na malalamiko yanayoweza kujitokeza.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Prof. Janabi pia aliwahimiza wafanyakazi wa Taasisi hiyo kuendelea kutunza vizuri kumbukumbu mbalimbali zikiwemo za wagonjwa na utendaji wa kazi zao za kila siku ili pale zitakapohitajika zipatikane kwa haraka.
“Mjitahidi kujaza fomu ya wazi ya mapitio na upimaji utendaji kazi (OPRAS) kwa wakati ili kusiwe na malalamiko ya upandaji wa vyeo kwani ujazaji wa fomu hizo ndiyo unaowezesha mfanyakazi kupimwa utendaji wake kwa kipindi cha mwaka mzima”, alihimiza Mkurugenzi Mtendaji huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Godfrey Tamba aliupongeza uongozi wa Taasisi hiyo kwa kazi wanayoifanya ya kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi zao katika mazingira bora.
Tamba alisisitiza, “Wafanyakazi wenzangu tunaodai haki zetu tukumbuke kutimiza wajibu wetu wa kazi kwa wakati, kwani uongozi wa TUGHE hautawatetea watu ambao hawatimizi wajibu wao ipasavyo”.
Hiki ni kikao cha pili cha wafanyakazi wote kufanyika tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo katika kikao hicho mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.




0 Comments