NA WAMJW-RUKWA .
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii,jinsia ,Wazeee na watoto
Ummy Mwalimu amemuagiza Mganga mkuu wa mkoa wa rukwa
kuboresha huduma za afya katika ngazi zote ili kuwasaidia wananchi wa mkoa huo
kulingana na sera ya afya.
Hayo ameyasema leo wakati wa ziara yake ya kukagua huduma za
Afya katika Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa.
Maelekezo yangu ni tujenge hospitali zetu za Wilaya
kwasababu pia idadi ya watu inazidi kuongezeka hivyo zitasaidiana na zile za
taasisi zisizo za kiserikali ili kutimiza sera na miongozo ya Serikali?
Aidha Waziri Ummy amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kufuatilia
kwa ukaribu huduma zitolewazo na
hospitali za taasisi zisizo Zakiserikali ili kuhakikisha kwamba
zinafuata miongozo na sera ya Afya ya Serikali.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface
Kasulu amesema kuwa kuna changamoto
mbali mbali zinazoikumba Mkoa wake zikiwemo
upungufu wa watumishi wa Afya kwani Mkoa unahitaji jumla ya watumishi 3489
lakini waliopo ni watumishi 1593 sawa na 46% huku kukiwa na upungufu wa watumishi
1895 ambayo ni sawa na 54%.
Aidha Dkt. Boniface amesema kuwa licha ya changamoto zilizopo ameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kupitia
Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na ushirikiano na
wadau mbalimbali kwa kuwajengea vyumba vya upasuaji katika vituo tisa huku
vituo sita vikiwa vinamilikiwa na Serikali jambo linalosaidia kupunguza vifo
vitokanavyo na kukosa upasuaji kwa muda.
Mbali na hayo Dkt. Boniface Kasulu amempongeza Mh. Rais wa
Tanzania Dkt. John Pombe magufuli kwa kuwapatia magari mawili ya kubebea
wagonjwa jambo ambalo limesaidia kupunguza hadha ya hospitali nyingi ikiwemo
vifo vya mama wajawazito
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii,jinsia ,Wazeee na watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo.




0 Comments