Baadhi ya Wazee wa
wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni nje ya Ofisi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi, wakisubiri kuwasilisha Kero zao.
Baadhi ya Wakazi wa
wilaya ya Ilala waliofika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
kuwasilisha Kero zao kwa Mhe. William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William lukuvi ameendelea na zoezi la kusikiliza
kero za wananchi mkoani Dar es salaam ,ambapo leo alikuwa akisikiliza kero za
wananchi wa wilaya ya Ilala.
Zaidi ya Wananchi
elfu moja wamesikilizwa kero zao katika zoezi hilo. Aidha, Mhe. Waziri ametoa tahadhari ya aina
nyingine ya utapeli; ambapo ameeleza kuwa matapeli wamekuwa wakighushi barua za
toleo/ Offer Letter za wananchi.
Mhe. Lukuvi amesema
kuwa imebainika kuwa kuna Matapeli ambao wamekuwa wakishirikiana na maafisa
ardhi ambao sio waaminifu na wamekuwa wakitumia barua za toleo za wananchi wa
kipato cha chini kwa kutengeneza barua za toleo nyingine kwa viwanja ambavyo vimeshakwisha milikishwa.
Amesema matapeli hao
hutumia majani ya chai ili kuchakaza barua hizo ili zionekane chakavu kuliko
zile za awali.
Aidha; Wananchi waliohudumiwa
leo wamepongeza hatua za Mhe. Lukuvi katika kutatua changamoto zinazowakabili
kwani wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.
Na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi
0 Comments