Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese
akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha shughuli
za kilimo na elimu kwa wananchi.
Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika
halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Godwin Everygist akifafanua jambo kwa
wananchi wakati wa uhamasishaji wa shughuli za kilimo.
Ofisa Elimu Sekondari halmashauri ya wilaya ya
Kishapu, Stephen Cleophas akihamasisha wananchi kushiriki shughuli za elimu.
Ofisa Elimu Msingi halmashauri ya wilaya ya
Kishapu, Moshi Balele akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji
elimu na kilimo kwa wananchi.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi
wa kampeni hiyo kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi wilayani Kishapu.
.................................
Na Mwandishi Maalumu, Kishapu
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
imezindua kampeni kabambe ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za
kilimo na elimu.
Imezindua kampeni hiyo katika kijiji cha Malwilo
kata ya Somagedi ambayo itashirikisha wananchi katika vijiji vyote vya wilaya
hiyo ili kuinua hali za wananchi kiuchumi na kielimu.
Akizindua kampeni hiyo wa niaba ya Mkuu wilaya
hiyo, Nyabaganga Taraba, Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese alisema kila
mwananchi ana wajibu wa kutumia fursa ya ardhi kujiletea maendeleo.
Kengese alimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili
hali ya ukame kutokana na hali ya hewa ya wilaya hiyo ambayo hupata mvua chini
ya wastani unaotakiwa.
Alisema halmashauri ya wilaya hiyo kwa kutambua
hali ya hewa ilitunga sheria ndogo mwaka 2008 ya kilimo cha mazao
yanayostahimili ukame na hifadhi ya chakula cha kutosha kwa kaya.
“Sheria hii imemtaka kila mkazi wa wilaya ya
Kishapu kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwa ni pamoja na kuhifadhi chakula
cha kutosheleza mahitaji ya familia angalau miaka miwili au zaidi.
“Aidha sheria hii ilitungwa ili kutuhakikishia
usalama wa chakula muda wote hivyo ni rai yangu kuwa wananchi wote tutashiriki
katika shughuli za kilimo kwa kulima mazao yanayostahimili ukame,” alisisitiza.
Aidha, Kengese aliongeza kuwa sheria imetaja
adhabu kwa mtu atakayekadi adhabu yake ni kifungo kisichozi miezi 12 au kulipa
faini isiyozidi sh. laki tatu au adhabu zote mbili.
Pia aliwataka maofisa kilimo waisimamie sheria
hiyo kikamilifu na kuwa yeyote atakayekaidi afikishwe kwenye vyombo vya sheria
kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.
0 Comments